
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na washiriki wa kongamano
la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii
leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.

Mhadhiri
wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria akielezea hali ya vyuo
vikuu vya Afrika katika muktadha wa Kimataifa wakati wa kongamano la
kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo
Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.

Baadhi
ya washiriki wa kongamano maalum la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa
kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mhadhiri wa
Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria wakati akielezea hali ya
vyuo vikuu vya Afrika katika muktadha wa Kimataifa mapema hii leo Chuo
Kikuu jijini Dar es Salaam.

Rais
Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Waziri
Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) wakati wa kongamano la
kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
mapema hii leo Chuoni hapo, katikati ni Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade
Aina toka nchini Nigeria.

Rais
Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na
Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Wakuu wa Vitivo wa Chuo
hicho wakati wa kongamano la kusherehekea kutimiza miaka 55 toka
kuanzishwa kwa chuo hicho.
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
...................................................................................................................
Na: Frank Shija, MAELEZO.
UONGOZI
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) takiwa kuhakikisha Chuo hicho
kinaendelea kuwa kiongozi miongoni mwa Vyuo Vikuu nchini.
Ushauri
huo umetolewa na Rais mstaafu wa awamu ya Nne ambaye pia ni Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
alipokuwa akifungua maadhimisho ya miaka 55 ya chuo hicho leo Jijini Dar
es Salaam.
“Hiki
ndicho Chuo kiongozi kati ya Vyuo Vikuu vyote hapa nchini, mnatakiwa
kuhakikisha kinaendelea kuwa kiongozi huku Vyuo vingine vikifuatia”.
Alisema Dkt. Kikwete
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa
Lwekaza Mukandara amesema kuwa pamoja na changamoto zinazo kikabili chuo
hicho wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kusaidia katika kuleta
maendeleo ya chuo hicho.
Alisema
kuwa baadhi ya changamoto zimetatuliwa kwa pamoja kati ya Serikali na
wahisani ambapo alisema kuwa ujenzi wa kumbi mpya za mihadhara, Maabara
za Kisasa na jengo la malazi,pamoja na ujenzi wa hosteli za wanafunzi
unaoendelea katika Kampasi ya Julius K. Nyerere ambayo itakuwa na uwezo
wa kutumiwa na wanafunzi 4000 mara itakapo kamilika.
Akiwasilisha
mada juu ya “hali ya Taaluma Barani Afrika katika Muktadha wa
Kimataifa” Mhadhiri wa Heshima kutoka nchini Nigeria, Profesa Tade Aina
amesema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni moja kati ya Vyuo Vikuu
mahiri barani Afrika ambapo kimetoa mchango mkubwa kwa ukombozi wa nchi
nyingi za bara hili.
Aliongeza
kuwa yeye binafsi ni mnufaika mkubwa wa UDSM kwani amekuwa na
ushirikiano mkubwa na baadhi ya wahadhiri kutoka chuo hicho katika
masuala mbalimbali ya taaluma.
Jaji
Mstaafu Joseph Sinde Warioba ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wakati wa
uwasilishaji mada alisema kuwa kipindi Chuo hiki kinaanzishwa aina ya
masomo yaliyokuwa yanafundishwa chuoni hapo yalikuwa na muelekeo kuandaa
wafanyakazi wa Serikali kwa wakati huo.
Na
kuongeza kuwa muelekeo wa aina ya masomo uliendelea kubadilika kadri ya
siku zilivyokwenda kutokana na mabadiliko ya teknolojia na uhitaji wa
soko la ajira.
Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam kinaadhimisha miaka 55 tangu kuanzishwa kwake
mnamo mwaka 1961 kikiwa ni tawi la Chuo Kikuu cha London, ambapo awali
kilianzia katika mtaa wa Lumumba kikiwa na wanafunzi 14 kabla ya
kujengwa mahali kilipo sasa katika eneo la Mlimani.