Mkurugenzi
wa Habari, Hassani Abbas (kulia) akizungumza jambo na Mwandishi
Mwadamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Mashaka Mgeta (kushoto) wakati wa
ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa
kazi leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mhariri Mtendaji Anicetus
Mwesa.
Mkurugenzi
wa Habari, Hassani Abbas (kushoto), akizungumza na Wahariri Waandamizi
wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa (katikati), Exuper Kachenje na
Kizito Noya wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja
na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
wa Habari, Hassani Abbas (kushoto), akizungumza na Wahariri Waandamizi
wa Gazeti la Jambo Leo, Joseph Lugendo (kushoto), na Joseph Kulngwa
wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti pamoja na kubadilisha
uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas (katikati) akizungumza na Bodi ya Uhariri ya
gazeti la Jambo Leo wakati wa ziara wakati wa ziara ya kutembelea ofisi
za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es
Salaam.

Mkurugenzi
wa Habari, Hassani Abbas (kulia) akipokelewa na Kaimu Mhariri Mkuu wa
gazeti la Majira, Eckland Mwaffisi wakati wa ziara ya kutembelea ofisi
za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es
Salaam.

Mhariri
Mtendaji wa Gazeti la Majira, Imma Mbughuni akimkaribisha Mkurugenzi wa
Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo
pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas akizungumza na watendaji wakuu wa gazeti la
Majira, akiwemo Mhariri Mtendaji, Imma Mbunghuni wakati wa ziara ya
kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Jonas Kamaleki.

Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
watendaji wakuu wa gazeti la Majira, Imma Mbughuni (kulia) na Kaimu
Meneja Mkuu wa kampuni ya Bussines Times Ltd Sophia Mshangama (kushoto).
...................................................................................................................................
Na Beatrice Lyimo
SERIKALI
imevitaka wadau wa vyombo vya habari nchini kuacha kulalamika na badala
yake waendelee kutoa maoni yao kuhusu muswada wa sheria kwa vyombo vya
habari ambao unatarajiwa kuwasilishwaa katika Bunge lijalo mjini Dodoma.
Akizungumza
katika wakati tofauti wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi za
Vyombo vya habari nchini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO),
Hassan Abbas alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa muswada huo
unapitishwa na Bunge ili uweze kuwa sheria kamili na hatimaye kuifanya
tansia ya habari kuzidi kuheshimika.
Mkurugenzi
Abbas alisema tangu muswada huo uliposomwa kwa mara ya kwanza Bungeni,
mwezi Septemba mwaka huu, wadau wa tasnia ya habari nchini ikiwemo
Wahariri na waandishi wa habari wamekuwa mstari wa mbele kupingana
katika mitandao ya kijamii badala ya kutoa maoni yao katika mamlaka
zinazohusika.
“Ni
aibu kwa maoni ya muswada huu yanayohusu tasnia ya habari kutolewa na
watu ambao hawana taaluma ya habari, hivyo tukiwa kama wanataaluma ni
vyema tujitokeze kwa wingi kutoa maoni kifungu kwa kifungu ili kuweza
kuboresha muswada” alisema Mkurugenzi Abbas.
Aliongeza
kuwa haitopendeza kwa muswada huo kuendelea kutolewa maoni na wananchi
wengine na wadau wa muswada kukacha kutoa maoni yao, na hivyo
kusababisha muswada huo kuandikwa na watu walio nje ya tasnia ya habari.
Abbas
alisema, muswada huo utakusudia kuiongezea nguvu tasnia ya habari kwa
kuweka ikiwemo suala zima la kuzingatia sheria na mipaka ya nchi katika
utoaji wa habari na taarifa maalum za Serikali kwa umma kwa kuzingatia
ukomo wa kimataifa.
“Azimio
la Umoja wa Mataifa la mwaka 1948, pamoja na kuzungumzia kuhusu haki ya
kupata taarifa lakini pia limeanisha sheria mbalimbali ambazo hazina
budi kuheshimiwa, na sheria hizo ni pamoja na sheria za ulinzi na
usalama” alifafanua Mkurugenzi Abbas.
Akifafanua
zaidi alisema taaluma ya habari ni tasnia muhimu katika maendeleo ya
taifa ila kwa upande mwingine inaweza kuharibu maendeleo kwa njia moja
au nyingine na hivyo kuwataka wadau wa habari kujitokeza kutoa maoni kwa
kujenga hoja za msingi ili kuboresha muswada badala ya kulalamika.
Aidha
kwa upande mwingine, Abbas alisema Ofisi yake ni mlezi na mratibu wa
vyombo vya habari na hawana budi kuwasiliana naye pindi wanapopata
changamoto mbalimbali ikiwemo utoaji na upatikanaji wa taarifa za
Serikali katika Wizara, Taasisi, Idara, Mikoa na halmashauri nchini.
Pia
alisema zipo taarifa ambazo zinahitaji kufanyiwa uhakiki ikiwemo ufundi
na takwimu, na hivyo aliwataka waandishi wa habari kuwa wavumilivu pale
wanapohitaji taarifa hizo kutoka kwa maafisa habari wa Wizara au
Taasisi husika.
Kwa
upande wake, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Majira, Imma Mbughuni
alisema chombo hicho kimejipanga kutoa maoni yao kuhusu muswada huo na
mara baada ya kumaliza wanatarajia kuwasilisha katika kamati ya kudumu
ya Bunge.
Naye
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa alisema chombo
chao pia kimekusudia kuupitia muswada huo ili kutoa maoni yao na baadae
kuyawasilisha katika kamati husika..