Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Pili kulia) akiongea na wanafunzi wa
kidato cha pili katika Sekondari ya Lake Natron alipotembelea Shule hiyo wakati
wa ziara ya Kikazi inayoendelea Katika
Wilaya ya Ngorongoro. Rc Gambo alimpongeza Mkuu wa shule hiyo kwa uwajibikaji
na kujitoa katika kuongoza Shule hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha (kwanza kulia) akitoa maelekezo wakati anakagua ujenzi wa
madarasa manne katika Shule ya Sekondari Lake Natron iliyopo Wilayani
Ngorongoro. Rc alizidi kuwapongeza kwa usimamiaji makini wa mradi huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha (aliyevaa masai shuka) akiwasili katika Kijiji cha Pinyinyi
kwenye Mkutano wa Hadhara na wananchi wa
eneo hilo . Wananchi walimshukuru Rc wa Arusha kwa kufika katika eneo hilo
baada ya kusahauliwa na viongozi kwa zaidi ya miaka kumi. Rc wa mwisho kufika katika Kata hiyo ni
Mohamed Babu mwaka 2005.
Rc
Gambo akiongea na wananchi wa Kijiji cha Pinyinyi kwenye Mkutano wa hadhara. Wananchi
hao wameomba msaada wa haraka kwa tafiti
na tiba ya ugonjwa wa ajabu unaowasumbua
wa kutapika Damu na mpaka sasa umesababisha vifo 21.
Wananchi wa Kata ya Digodigo (wazee) ambao
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametoa Fedha kwa ajili ya kujiunga na huduma ya
Tiba kwa Kadi (Tika) chini Mfuko wa Bima
ya Afya. Rc aliendesha zoezi la kuhamasisha
wananchi kujiunga na kila aliyeambatana naye kwenye Msafara wake
alimtaka kuchangia wananchi 2-6 kujiunga na Tiba kwa Kadi. Idadi ya Kaya 127
zimefanikiwa kujiunga na Tika kupitia zoezi hili.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega akiwa na wananchi wake ambao
anawachangia Fedha kwa ajili ya kujiunga na Tika.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Methew Silomba(kulia) akiwakabidhi
wananchi wake Fedha za kujiunga na Tika katika zoezi la kuhamasisha kujiunga na
mfuko huo lililoendeshwa na Mkuu wa Mkoa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi
wa Digodigo
Mkuu
wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Rashid Mfaume Taka (kulia) akifunga Mkutano wa
hadahara uliofnyika katika Kata ya Digo Digo.
1 Wananchi
wa Kata ya Digo Digo waliohudhuria Mkutano wa hadhara na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mhe. Mrisho Mashaka Gambo.
.....................................................................................................................
Nteghenjwa
Hosseah - Arusha
Wananchi wa Kata Pinyinyi, Wilaya ya
Ngorongoro wanasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu wa kutapika damu kwa takribani miaka
minne sasa na hali hii imewasababisha wananchi hao kuwa na hofu na kukosa amani
ya kuendelea kuishi katika makazi yao.
Wakiwasilisha kero zao mbele ya Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ambaye yuko katika ziara ya Kikazi kwenye Wilaya
hiyo wananchi hao wamesema mpaka sasa wananchi zaidi za ishirini wamefariki dunia
kutokana na ugonjwa huo ambao mpaka sasa hawafahamu kwamba ni ugonjwa gani.
“Ugonjwa huu ulianza tangu 2012 na mgonjwa
huwa anatapika damu kwa kipindi kirefu na baadae hufariki na sisi kama wananchi
wa Kijiji hiki tulishapeleka taarifa hizi kwa Halmashauri ya Wilaya na wakaja
mpaka hapa kijijini lakini ufumbuzi wa ugonjwa huu haujapatikana kutokana na
kutokua na majibu sahihi ya chanzo na aina ya ugonjwa huu” alisema Zakayo
Siranga mkazi wa Punyinyi.
Aliongeza kwa kusema kuwa wagonjwa wa aina hii
wakienda kutibiwa katika Hospital zetu hawaponi lakini kuna wachache
waliokwenda Nchi jirani ya Kenya kupata matibabu walipona sasa hatuelewi nini
ambacho kimeshindikana katika Hospital zetu tunaomba Serikali itusaidie.
Akijibu hoja hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Ngorongoro Dr. Omary Sukari amethibitisha kuwepo kwa ugonjwa huu na alieleza
jitihada ambazo zimefanyika kutafuta ufumbuzi wa ugonjwa huu na kuwa wamekwisha
chukua sampuli ya damu na kupeleka kwenye Taasisi ya Utafiti Magonjwa wa
magonjwa ya Binadamu(NIMR) lakini mpaka sasa hawajapata majibu kutoka katika
Taasisi hiyo.
Rc Gambo alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa Dr.
Frida Motiki kutuma wataalamu ndani ya wiki hii wa kufanya tafiti ya ugonjwa
huo hatari na kupeleka tena sampuli hiyo NIMRI ili kupata taarifa sahihi na
kutafuta ufumbuzi wa haraka.
“Ugonjwa huu ni hatari sana na sisi kama
Serikali hatuwezi kukaa Kimya kwa sababu unagharimu uhai wa watu, kwa takwimu
hiyo ya watu 21 kufariki ni kitu cha kusikitisha sana hivyo nahitaji kupata ufumbuzi wa ugonjwa huu kupitia kwa
wataalamu wangu wa Afya”.
Kata ya Pinyinyi haijawahi kutembelewa na Kiongozi wa Ngazi ya
Mkoa kwa zaidi ya miaka kumi sasa wananchi hao walitoa shukrani zao kwa Mkuu wa
Mkoa Mhe.
Gambo kwa kuanzia ziara yake
katika Kata hiyo na kueleza kwamba wanaona sasa wao ni sehemu ya wananchi
halali wa Mkoa huu kwa kuwa walikua wamesahaulika kwa kipindi kirufu na wana
imani kero zao sasa zitapata ufumbuzi wa haraka.









0 Comments