Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega
akikagua jengo linalotarajiwa kuwa shule mpya katika kitogoji cha kikonga
katika ziara yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja
kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupu Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega
akizungumza na wananchi katika kitongoji cha Kikonga akiwa ziara yake kijiji
kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja na kuangalia maendeleo
leo katika Kijiji cha Bupu Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah
Ulega akizungumza katika mkutano wa wananchi wa kitogoji cha Kikonga juu ya
changamoto zinazowakabili akiwa ziara yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuu
wananchi kwa kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupu
Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah
Ulega akiwaonyesha wananchi Diwani wao,Abbas Msangule jinsi ya kushirikiana
naye kwa maendeleo katika Kijiji cha Kondo Mwelazi katika ziara yake kijiji kwa
kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo
katika Kijiji cha Bupu Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega
akiwa katika picha ya pamoja na walimu
wa shule ya msingi Kondo Mwelazi alipowatembelea kujua mazingira
walionayo na kuwashukuru kuendelea na
moyo licha ya kuwa na mazingira mgumu leo.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya
Jamii
................................................................................................................
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega
amewataka wananchi kufanya maendeleo na sio siasa kwa muda huu.
Hayo ameyasema leo katika katika
ziara ya vijiji vya kata ya bupu, Ulega amesema kuwa wakati umefika kwa kabila
yake kusomesha watoto kwa ajili ya maendeleo kutokana dunia ya sasa inahitaji
watalaam.
Ulega amesema kuwa changamoto zilizo
katika kata ya Bupu ni maji pamoja na miundombinu ya barabara hivyo vinatakiwa
kupatiwa ufumbuzi ili wananchi waondokane na changamoto hizo.
Mbunge huyo ameahidi kutoa Bati 50
katika shule mpya inayojengwa katika kitongoji cha kikonga kutokana watoto wa kitongoji hicho wanatembea
kilomita sita.
Ulega amesema changamoto zilizopo
wilaya ya mkuranga zinatakiwa zitatuliwe kutokana na kuomba kazi ya kuwatumikia
wananchi.
Amesema kuwa suala mfuko wa afya ya
jamii CHF dawa hazipatikani na kufanya wananchi wengine washindwe kujiunga.
Aidha amesema wananchi waliojiunga na
CHF ni 65 ikiwa nia serikali ni watu wote wajiunge ili wasipate adha ya kupata
huduma za afya.
Hata hivyo amesema nia ya Rais Dk.
John Pombe Magufuli ni kuona wananchi wanafurahia huduma zinazotolewa na
serikali na sio vinginevyo.
waakuu mdawenu





0 Comments