Naibu Waziri Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na serikali za
mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza
na watumishi wa Halmashauri ya Ingunga, Tabora.
..................................................................................................
KUTOKANA
na baadhi ya wananchi kuwafanyia vitendo vya ushirikina watumishi katika
Halmashauri mbalimbali nchini, Naibu Waziri Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na
serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ameonyeshwa kukerwa na tabia hiyo
huku vimesababisha watumishi kupata msongo wa mawazo na wengine kuomba
kuhamishwa.
Jafo
alitoa kauli hiyo alipokuwa akikagua zahanati mpya iliyopo kijiji cha Ziba
ndani ya Jimbo la Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora na alipokuwa
akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo.
Alimuagiza
mkuu wa wilaya ya Igunga kutenga muda yeye na kamati yake ya ulinzi na usalama
kuwafikishia ujumbe wananchi wa wilaya ya Igunga kuwakemea wenzao wenye tabia
hiyo wilayani humo ili kuacha tabia hiyo ovu.
Jafo alisisitiza kwamba tabia hiyo
imewasababishia baadhi ya watumishi walio tendewa vitendo visivyo kupatwa na
msongo wa mawazo na kuomba kuhama maeneo walio pangiwa.
Naibu
Waziri alisema kwamba jamii inapaswa kuwathamini watumishi kwani wametoka
maeneo mbalimbali ya nchi ili kuja kuwatumikia wao hivyo wanatakiwa kuwathamini
na kuwaheshimu kwa kulinda utu wao.
"
Watani zangu mliopo hapa Wasukuma na Wanyamwezi mmepata zahanati nzuri naomba
muitunze. Pia sitaki kusikia daktari au mhudumu amelala asubuhi anajikuta
ng'ambo ya barabara au katika kiwanja cha mpira,”alisema Jafo
Kadhalika,
alikemea kitendo cha sungusungu walio mchapa viboko mwalimu mkoani humo huku
akiwaagiza wakuu wa wilaya maeneo yote kupambana na tabia za udhalilishaji
wanazo fanyiwa watumishi wa umma katika jamii ili waweze kufanya kazi kwa amani
na kujiamini.
Aliwapongeza
viongozi wa mkoa wa Tabora kwa umoja na ushirikiano wao katika kuwaletea
maendeleo wananchi wa mkoa huo.

0 Comments