![]() |
| Mbunifu maarufu wa mitindo kutoka nchini Nigeria, Femi (wa pili kushoto), pamoja na mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano (wa kwanza kulia) wakiwa katika pozi pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania, kwenye maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanyika katika duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kulia) akigonganisha glasi ya mvinyo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo. |
WABUNIFU wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi wamejitokeza kufanya maonesha ya mavazi
mbalimbali
ya maharusi katika uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi
'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar
es
Salaa. Uzinduzi huo uliofanyika jana eneo la Sinza Madukani ulipambwa
na mbunifu wa mitindo kutoka nchini Nigeria ajulikanaye
kwa jina la Femi, mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini
Tanzania.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa ambao ni waandaaji wa onesho
alisema waliamua kufanya onesho hilo ili kutoa fursa kwa wananchi hasa wanaoelekea kufanya harusi kujua mitindo mbalimbali ya
mavazi ambayo wanaweza wakaitumia katika shughuli zao za harusi na kuonekana tofauti kimuonekano.
Alisema
wabunifu walifanya maonesho ya mavazi katika mitindo mbalimbali kutumia
mavazi ya hali zote ikiwa ni kuonesha jamii harusi
si lazima muhusika au maharusi kutumia gharama kubwa bali wanaweza kutumia gharama za chini na kuonekana wenye mvuto kama
watapata ushauri kutoka kwa wabunifu na wanamitindo.
Alisema duka lao pamoja na kuuza nguo za maharusi watakuwa wakitoa ushauri bure kwa maharusi endapo watafika katika duka hilo
ambalo
limekuja kuleta mabadiliko katika mitindo ya maharusi. Alisema duka
hilo litahudumia watu wenye kipato cha chini, cha kati na
hata cha juu kulingana na mahitaji ya wahusika huku wakinufaika kwa ushauri bure kila atakaetembelea na kuomba ushauri kwa
wataalamu wa mitindo.
Alisema
duka hilo kubwa la mitindo ya maharusi wa kike na kiume linatumia
wataalamu wa mitindo kutoka nchi za Uturuki, Marekani,
Italia pamoja na Tanzania. Alisema wamekuja kuondoa dhana iliyojengeka kuwa nguo za maharusi ni anasa kutoka na maduka mengi
kuuza bei kubwa kuliko inavyotegemewa, hivyo kupitia kwa wataalam wao maharusi wanaweza kufanya shughuli kwa bei ndogo na
kuvutia.
"...Watu wengi wanaona mavazi ya maharusi ni kama anasa kutokana na bei kubwa za mavazi haya, sisi tumeamua kuleta mabadiliko
hapa dukani kuna nguo za makundi yote, yaani watu wa kipato cha chini, watu wa kipato cha kati na hata watu wa kipato cha
juu...unaweza
kuandaliwa nguo yako ya harusi na wanamitindo kutoka nchi tulizotaja
wewe ukiwa hapa hapa nchini na ukaipata ndani
ya siku 21.
Akizinduwa duka hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang, Emelda Mwamanga alimpongeza mwanamama
mjasiliamali na mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo kwa uamuzi wa kusaidia kutoa ushauri kwa maharusi jambo ambalo limekuwa
likipasua vichwa kwa wahusika. Alisema kitendo hicho kinatoa changamoto kwa akinamama wajasiliamali kuweza kufanya mambo
makubwa kibiashara.









