
Katikati
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina, Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiru, na
Bwana Daniel Sagata Pamoja wakijiandaa kuanza zoezi la usafi wa
mazingira katika eneo la Binzatana Mjini Shinyanga mapema leo.

Naibu
Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luahaga Mpina
akishiriki katika zoezi la kupanda miti Mjini Shinyanga leo.

Viongozi pamoja na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga katka zoezi la usafi wa mazingira mjini Shinyanga leo.

Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina
akiongea na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyaga katika eneo la
Binzanata baada ya kukamilisha zoezi la usafi wa mazingira na kupanda
miti mapema leo.

Baadhi ya wakazi wa Mji wa Shinyanga wakishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira leo, Mjini Shinyanga.
..............................................................................................
EVELYN MKOKOI SHINYANGA
Uongozi
wa mkoa wa Shinyanga kupitia Mkuu wa Wilaya yake Bi Josephine Matiru
umeiomba serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Kujenga kiwanda
kitakacho tengeneza mkaa utokanao na mabaki ya miti ambao ni rafiki kwa
mazingira ili kunusuru hali ya mkoa huo kuendelea kuwa jangwa kutokana
na ukataji miti ovyo kwa matumizi ya makaa manyumbani, matumizi mengine
na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Mkuu
wa wilaya hiyo ametoa ombi hilo leo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina aliposhiriki siku
ya usafi kitaifa ya mwisho wa mwezi October ambapo zoezi hilo
lilizinduliwa rasmi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania December
Mwaka jana na kuendelea kutekelezwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi
kama siku maalum ya usafi nchini.
Bi
Materu aliendelea kusema kuwa, Mkoa wa shinyanga unakumbana na
changamoto kubwa ya ukataji miti ovyo ambayo ingeweza kukabiliwa kwa
kutumia mabaki ya miti, taka na maranda ya mbao kutengeneza mkaa rafiki
kwa mazingira na kusema kuwa mkoa na wilaya ya shinyanga imebarikiwa
kuwa na miti ya aina mbali mbali ambazo mazingira yangetunzwa vizuri na
kutumia malighafi hiyo ya taka kutengeneza mkaa banifu akitolea mfano
kiwanda cha kutengeneza mkaa rafiki wa mazingira cha Zanzibar.
Kwa
Upande wake Naibu Waziri Mpina alikiri kupokea maombi ya mkuu wa wilaya
huyo na kueleza kuwa serikali itakuwa tayari kujenga kiwanda cha
kutengeneza mkaa mjini shinyanga “Na pengine katika Mbio za Mwenge
Mwakani tukijaaliwa tunaweza kuzindua kiwanda hicho kama mradi wa
mfano.” Alisisitiza Mpina. “Lazima tuwe na viwanda vya mkaa rafiki kwa
mazingira sasa na wafanya biashara wa gas za manyumbani sasa ufike
wakati nao washushe bei ili asilimia kubwa ya watanzania waweze kutumia
nishati hiyo.” Alifafanua Mpina.
Akizungumzia
suala ya usafi wa Mazingira ambapo sambaba na hilo Naibu Waziri Mpina
Pia alishiriki zoezi la upandaji miti katika eneoa la Binzamata, alisema
kuwa watanzania wana kila sababu ya kujijengea utamaduni wa usafi wao
pamoja na mazingira kwani hata vitabu vitakatifu vinasisitiza usafi wa
mazingira akitolea mfano kitabu cha Biblia takatifu cha kumbu kumbu la
Torati 23:11-14 na kusema kuwa “Pahala Pachafu hapana Utukufu wa Mungu
na hauwezi kuonekana mahali hapo na haya siyo maneno yangu wala ya Rais
Magufuli, ni maneno ya biblia hivyo watendaji katika ngazi zote
mzingatie utekelezaji wa sheria yya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni
zake na kuwachulia hatua wale wote watakao kiuka sheria hiyo.”
“Ni
jukumu la kila mtu kufAnya usafi na kila wilaya na Halmashauri
ijetengenezee mwongozo na sheria ndogo ndogo katika eneo hili la usafi
wa mazingira na lazima watu wawajibike.”
Naibu
Waziri Mpina Pia alisisitiza zoezi la upandaji miti ili kuweza
kukabiliana na athari zitokanazo na Mabadiliko ya tabia nchi na
kurudisha uoto wa asili.
Akitolea
mfano wa kasi ya serikali ya awamu ya tano katika zoezi la usafi wa
mazingira Mpina alisema “ watu walidhani Mhe. Rais alivyozindua siku ya
usafi zilikuwa ni nguvu za soda, kasi tuliyonza nayo ndiyo tutakayo
maliza nayo, waharibifu wa mazingira lazima sheria iwashughulikie.”
Alisisitiza Mpina.
Akizungumzia
wananchi wanaoabudu siku ya Jumamosi Mpina alisema Sheria ndogo ndogo
za mazingira za Halmashauri na miji ni vizuri zikaona namna ya kuweza
kuwapa nafasi na wao ya kuabudu na kushiriki usafi katika siku hiyo.
Siku ya kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi imetengwa na serikali ikiwa ni maalum kwa ajili ya usafi nchini.
0 Comments