
WAZIRI
wa viwanda ,biashara na uwekezaji ,Charles Mwijage (mb),akisaini kitabu
kwenye banda la SIDO baada ya kuzindua maonyesho ya tisa ya
wajasiriamali mwaka 2016 ,yaliyoratibiwa na SIDO Kanda ya Mashariki
yanayofanyika wilayani Bagamoyo.

WAZIRI
wa viwanda ,biashara na uwekezaji, Charles Mwijage (mb),akitembelea
mabanda mbalimbali ya wajasiriamali waliojitokeza kuuza bidhaa zao
kwenye maonyesho ya tisa ya wajasiriamali mwaka 2016 yaliyoratibiwa na
shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo SIDO ,Kanda ya
Mashariki,yanayofanyika wilayani Bagamoyo.

Mkuu
wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza jambo kabla ya
kumkaribisha kuzungumza na wananchi waziri wa viwanda,biashara na
uwekezaji Charles Mwijage(mb)katika maonyesho ya tisa ya wajasiriamali
mwaka 2016 ,yaliyoratibiwa na SIDO Kanda ya Mashariki,wilayani Bagamoyo.

Waziri
wa viwanda,biashara na uwekezaji,Charles Mwijage(mb)akizungumza na
baadhi ya wananchi na wajasiriamali wilayani Bagamoyo,katika maonyesho
ya tisa ya wajasiriamali mwaka 2016 yaliyoratibiwa na SIDO,Kanda ya
Mashariki.


Waanachi
mbalimbali wakionekana kujitokeza kununua bidhaaa zilizotengenezwa kwa
mikono ya wajasiriamali kutoka ndani ya Tanzania kwenye maonyesho ya
tisa ya wajasiriamali mwaka 2016 ,yaliyoratibiwa na SIDO Kanda ya
Mashariki ,yaliyofanyika wilayani Bagamoyo.
(picha na Mwamvua Mwinyi)
................................................................................................................
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
WAZIRI
wa viwanda ,biashara na uwekezaji ,Charles Mwijage(mb),amesema wakati
serikali ikiendelea kusisitiza kukuza sekta ya viwanda na kuinua uchumi
wa kati ni lazima kuanza na ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati.
Aidha
ameitaka mikoa na wilaya kubaini na kutenga maeneo kwa ajili ya kujenga
viwanda pamoja na kuhamasisha wajasiriamali kuwa na uthubutu wa kujenga
viwanda .
Akizindua
maonyesho ya tisa (9)ya wajasiriamali mwaka 2016,yaliyoratibiwa na SIDO
,Kanda ya Mashariki,alisema mwaka 2013 viwanda vilivyokuwa vinafanya
kazi ni zaidi ya 49,243 sawa na asilimia 99.15 .
Mwijage
alisema kati ya viwanda hivyo ni vidogo sana,viwanda vidogo na vya kati
hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuongeza wigo wa kuwa na viwanda
hivyo kwenye maeneo mbalimbal .
Alieleza
kuwa kulingana na taarifa zilizowahi kutolewa na bank ya dunia ilieleza
kuwa nchi ya India viwanda vidogo ni asilimia 95.1 ambapo wajasiliamali
wadogo na viwanda vidogo wanachangia asilimia 38 la pato la taifa.
Mwijage
alisema Tanzania isije ikajibeza kwa takwimu za mwaka 2013 zilizopo
kwani nchi nyingi duniani zimekuwa kiuchumi na kuongeza pato la taifa
kutokana na viwanda vidogo na vya kati.
“Viwanda
vidogo katika nchi ya China ni asilimia 90 ,Malaysia asilimia
98,Thailand asilimia 99,Ghana asilimia 97 ,Afrika ya kusini asilimia
97.7 ,Marekani ni asilimia 98.8 na Japan ni asilimia 98.7 .
Alisema
ni lazima kulenga viwanda vidogo kwani vinapatikana kwa mitaji midogo
na vipo vijijini na watanzania zaidi ya 70 wapo vijijini hivyo kwa
kuwaondolea umaskini ni kuwapelekea viwanda na maendeleo.
“Wananchi
wengi watapata maendeleo kwa kulima na kuuza kwenye viwanda lakini
ukitumia nguvu nyingi na kwenda kuuza mjini kwa nusu gharama ujue
umepigwa vidole”
“Mkoa
wa Pwani unajenga viwanda vingi ikiwemo vya kusindika matunda,viwanda
vya kuchakata matunda ,kwa hiyo kuna uhakika wa kupanua wigo wa soko nje
na ndani ya nchi”alisema Mwijage.
Aliwaomba
wajasiliamali hao kufunga bidhaa kwa ubora, kuwa na mbinu mpya hasa
katika soko la ushindani hali itakayosaidia kukuza biashara na kupata
masoko makubwa.
Alisisitiza kwamba Tanzania bila ya viwanda inawezekana ni msemo wa zamani kwasasa ni Tanzania inajenga viwanda na inawezekana.
Mwijage
alieleza kikubwa ni kuainisha maeneo na viwanda vinavyojengwa katika
wilaya husika kulingana na taswira ya wilaya na mkoa.
Alisema
kikwazo kikubwa ni maeneo ya kufanyia shughuli ,na kuyaainisha kwani
kosa kubwa linalofanywa na halmashauri za wilaya nyingi ambazo
wanakimbilia kuyauza maeneo kwa kuyakata vipande na kuyauza kwa scare
mita1 sh 10,000 heka moja mil. 60 .
Waziri
huyo alisema vijana wanaotoka shule hawawezi kumudu gharama hizo hivyo
kunufaisha watoto wenye uwezo pekee na kuwakandamiza wale hohehahe na
hatimae kugeuka panyaroad .
Wakati
huo huo ,Mwijage alisema anatarajia kupeleka makatibu wake watatu
kwenda mikoani kuwasomea waraka wake wa waziri unalenga kuibua vijana
wanaotoka shule kujifunza teknolojia ili waweze kujitegemea.
Alisema
serikali za mikoa zisaidiane na serikali na ameahidi kuwapeleka katibu
mkuu anaeshughulika na viwanda ,katibu mkuu anaedhughulikia uwekezaji na
naibu katibu mkuu wa viwanda ,biashara na uwekezaji kwa ajili ya
kuusemea waraka huo.
Alisema
makatibu hao wataenda kushirikiana nao katika maeneo yaliyotengwa na
halmashauri ili kutamia vijana mbalimbali na endapo watakua wataendelea
kujitegemea.
Katika
hatua nyingine Mwijage,aliwaalika wajasiliamali waliojitokeza katika
maonyesho hayo kwenda kwenye maonyesho yanayotarajiwa kufanyika des 7
hadi des 11 mwaka huu,kwenye viwanja vya sabasaba.
Awali mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema mkoa huo umejipanga kuwa ukanda wa viwanda na uwekezaji.
Alisema
wakati jiji la Dar es salaam likiwa limejaa hakuna budi wakurugenzi na
wakuu wa wilaya mkoani humo wakaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya
uwekezaji.
Mhandisi Ndikilo alitoa rai kuboresha miundombinu kwenye maeneo ya wawekezaji ili kuwavutia kukimbilia mkoani hapo.
Nae
mkurugenzi wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO)prefesa
Injinia Silvester Mpanduji,aliiomba jamii na wadau wa kibiashara kujenga
tabia ya kununua bidhaa zinazotokana na ubunifu na mikono ya
watanzania.
Alisema ni faraja kununua bidhaa za nchini kwani hazinatofauti na zile za nje ya nchi na zinauzwa kwa gharama nafuu.
Profesa
Injiani Mpanduji,alisema SIDO ina mikakati mbalimbali ikiwemo madhubuti
ya kuinua (kutotoa)vijana wajasiliamali wenye ubunifu na kujiamini
katika soko la ushindani.
Alieleza
katika maonyesho hayo wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa ya kanda
hiyo ikiwemo Pwani, Morogoro, Lindi, Dar es salaam na Mtwara na kutoka
nchini Kenya wameshiriki kwenye maonyesho hayo.
Profesa Injinia Mpanduji,alisema kauli mbiu ya maonyesho hayo ni uchumi wa viwanda unategemea viwanda vidogo .
Alisema
maonyesho hayo yalianza octoba 26 hadi 31 ambapo yanatarajiwa kufungwa
na mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo.
0 Comments