Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkaribisha ofisini kwake Balozi
wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) kwa ajili ya kufanya
mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Norway na
Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar
es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Japan nchini,
Ian Myles (wapili kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake,
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano
kati ya Tanzania na Japan. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Balozi Simba Yahya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara
hiyo, Haji Janabi, na kulia ni Msaidizi wa Balozi huyo, Pascale Julien.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Norway
hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri
Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Norway.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Balozi wa India hapa
nchini, Sandeep Arya (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini
kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na India.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa
Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri
Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa
India nchini, Sandeep Arya (kulia) mara baada ya Balozi huyo kumaliza
mazungumzo na Waziri ambayo yalifanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo.
Mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano
kati ya Tanzania na India.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsindikiza Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura
(kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, yaliyofanyika ofisini kwa Waziri
huyo, jijini Dar es Salaam leo. Lengo la mazungumzo hayo ni kujadili masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi jirani ya Rwanda na Tanzania.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.







0 Comments