Na.Alex Mathias.
Timu
ya Alliance imeng'ara katika uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kirumba
baada ya kuwatandika vijana wa kocha Minziro,Singida United goli 1-0
mchezo wa Ligi Daraja la kwanza ukiwa ni wakundi C na kujitupa hadi
nafasi ya kwanza huu na kumaliza mzunguko wa kwanza.
Kabla
ya kukutana Singinda United walikuwa wanaongoza Ligi kwa pointi 16 huku
Alliance walikuwa na pointi 14 na kwa matokeo vijana wa jiji la Mwanza
wamefikisha jumla ya pointi 17 katika msimamo wa kundi hilo.
Kiujumla
mchezo ulikuwa mgumu kwa kila timu huku Singida wakiongozwa na
wachezaji wakongwe waliowahi kuwika katika Ligi Kuu Tanzania Nizar
Khalfa pamoja na mdogo wake na Rashid Gumbo wakati Alliance wanatumia
vijana wadogo na wengine wapo katika kikosi cha Serengeti boys chini ya
umri wa miaka 17.
Kundi
hilo ndilo linalotabiriwa kuwa ngumu kwa timu hizo mbili kuchuana
vikali ili kutafuta nafasi ya kupanda Ligi Msimu ujao kwani kwenye
msimamo unasomeka Alliance 17,Singida 16,Rhino 13,Panone 6 na Polisi
Dodoma 6.
TAZAMA MATOKEO MENGINE YA DARAJA LA KWANZA:
.Rhino 2-0 Panone
.Kiluvya 1-0 Friends
.Ashanti 1-1 Lipuli
.Transit Camp 2-2 Milambo
.Burkina Faso 0-1 Changanyikeni
.Mvuvuma 1-0 Polisi Mara
.Polisi Dodoma 0-1 Mgambo.
0 Comments