Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
.............................................
Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania bara inatarajia kuendelea kesho viwanja Sita timu
kutafuta alama tatu muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri wadau wengi
pamoja na wapenda soka watakuwa wanaangalia viwanja vya Uhuru jijini Dar
es salam pamoja Sokoine mjini Mbeya bila kusahau uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
Katika jiji la Dar es salaam kutakuwa
na wenyeji wa Dar timu ya African Lyon itapambana na Simba kwenye Uwanja
wa Uhuru, mchezo Na. 144 wakati Mbao FC itakuwa mwenyeji wa Azam
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mchezo Na. 116.
Mkoani Mtwara kutakuwa na vita ya
wenyeji Ndanda FC watakowaalika wapiga debe toka Shinyanga timu ya Stand
United ambayo imetoka kujiruhiwa na Mnyama Simba kwa kufungwa goli 1-0
mchezo Na 117 huku Mjini Mbeya kutakuwa na pambano la kukata na shoka
wenyeji Tanzania Prisons itacheza na mabingwa watetezi Yanga
waliojeruhiwa na Mbeya City kwa kuchezea kichapo cha magoli 2-1 kwenye
Uwanja wa Sokoine mchezo Na. 118.
Baada ya kupata ushindi mjini Mwanza
dhidi ya Mbao FC Kagera Sugar watacheza na Ruvu Shooting kwenye uwanja
wa Kaitaba mjini Bukoba mchezo Na. 119 wakati wachovu wa Ligi timu ya
wanajeshi JKT Ruvu itawaalika wachovu wenzao toka Mwanza Toto African
‘Wana-kisha Mapanda’ kwenye uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani
Pwani mchezo Na. 120.
Hata hivyo Ligi hiyo itaendelea tena
Siku ya Jumatatu kwa michezo miwili , Mtibwa Sugar itawakaribisha
wababe wa Yanga kutoka Mbeya timu ya Mbeya City kwenye uwanja wa
Manungu uliopo mkoani Morogoro mchezo Na. 113na Mwadui FC baada ya
kupata kichapo kwenye uwanja wao dhidi ya Mtibwa Sugar watakuwa nyumbani
tena kucheza na vijana wa Kally Ongala timu ya Majimaji inayosuwasua
kwenye msimamo kwenye Uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga mchezo Na.
115.
0 Comments