Na
Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.
Benki
Kuu ya Tanzania (BOT) imesitisha kuweka dhahabu kama hazina ya rasilimali za
kigeni kwa sababu ya kuyumba kwa bei ya madini hayo katika soko la dunia na
kusababisha uwezekano wa kupunguza thamani ya hazina ya rasilimali ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu
Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga Mhe. Dalaly Kafumu
aliyehitaji kufahamu sababu za Serikali kukataa kutunza dhahabu safi katika
Benki Kuu wakati Tanzania ni nchi mojawapo inayozalisha dhahabu safi.
Mhe.
Kijaji amesema kuwa jukumu la msingi la Benki Kuu ni kuandaa na kutekeleza Sera
ya Fedha inayolenga kuwa na utulivu wa bei kwa ajili ya ukuaji endelevu wa
uchumi wa Taifa hivyo ili kufanikisha azma hiyo Benki Kuu inadhibiti ongezeko
la ujazi wa fedha kwa kutumia nyenzo mbalimbali zikiwemo za kuuza dhamana na
hati fungani za Serikali pamoja na kushiriki katika soko la jumla la fedha za
kigeni kati ya mabenki.
“Katika
kutekeleza jukumu lake la msingi, Benki Kuu hutunza hazina ya rasilimali za
kigeni zinazotosha kuagiza bidhaa nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne
lakini kwa muda mrefu sasa Benki Kuu ya Tanzania haiweki dhahabu kama sehemu ya
rasilimali hizo kutokana na kuyumba kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia”,
alisema Mhe. Kijaji.
Naibu
Waziri huyo ametoa mfano wa kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la Dunia
ambapo dhahabu ilishuka kutoka dola 1,745 za kimarekani katika mwezi Septemba
2012 hadi dola za kimarekani 1,068 kufikia mwezi Desemba 2015.
Mhe.
Kijaji amefafanua kuwa hazina ya rasilimali za kigeni zinaweza kuwa dhahabu –
fedha (monetary gold) au fedha za kigeni ambapo uamuzi kuhusu hazina itunzwe
vipi unazingatia vigezo mbalimbali vikiwemo vile vya kudumisha thamani, wepesi
wa kubadilisha pamoja na faida inayopatikana kwa kuwekeza hazina hiyo.
Aidha,
Mhe. Kijazi amesema kuwa ununuzi na uuzaji wa madini ya dhahabu unahitaji ujuzi
maalum ambapo kwa kuzingatia jukumu la msingi la Benki Kuu inaonyesha dhahiri
kuwa Benki hiyo haijajijengea uwezo katika eneo la biashara ya madini hayo.

0 Comments