Mabingwa
watetezi Yanga wamemaliza duru ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu
Tanzania bara kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting mchezo
uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Abrahman
Mussa alikuwa wa kwanza kuifungia Ruvu dakika ya 7 baada ya kuwazidi
ujanja walinzi wa Yanga chini ya Dante na Yondani licha ya kutanguliwa
goli hilo Yanga waliendelea kulishambulia lango wa Ruvu huku wageni
wakicheza mchezo wa kujilinda zaidi.
Haruna
Niyonzima alitoa pasi ya goli kwa Simon Msuva katika dakika ya 31 na
kuisawazishia Yanga baada ya kupata goli hilo Ruvu waliendelea kucheza
kwa kujilinda na kuruhusu mashambulizi mengi huku washambuliaji
Msuva,Ngoma,Chirwa na Tambwe wakishindwa kutumia nafasi vizuri hadi
mapumziko timu hizo zilienda nguvu sawa.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Yanga kupata pigo baada ya kocha wao Mkuu Hans
Van Der Pluijm,alitolewa nje ya uwanja kwa kuoneshwa kadi kutokana na
kutoa lawama nyingi kwa wamuzi wa mchezo huo licha ya kupata pigo
mabingwa hao waliendelea kutafuta pointi tatu muhimu.
Haruna
Niyonzima ambaye ndio alikuwa nyota wa mchezo aliifungia goli la pili
na la ushindi dakika ya 56 kwa shuti kali akipokea pasi ya Ngoma baada
ya kumtoka golikipa wa Ruvu hadi mwamuzi Mathew Akhrama toka Mwanza
anapuliza kipyenga cha mwisho Yanga wameibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Kwa
matokeo hayo Yanga wamefikisha pointi 33 na kuwa nyuma ya Simba wa
pointi mbili wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 35 na Ligi hiyo itasimama
na kuanza duru la pili mwakani Januari na huu mchezo kwa tetezi za chini
ulikuwa wa mwisho kwa Kocha Hans Van Der Pluijm ambaye atampisha
Mzambia Goerge Lwandamina.
0 Comments