Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto),
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na
Walemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia) na Katibu wa Bunge, Dkt.Thomas
Kashililah wakisubiri kupokea mwili wa Mbunge wa Dimani, marehemu
Hafidh Ally Tahir kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma ambako ulisafirishwa
kwenda Zanzibar kwa Mazishi Novemba 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na wabunge wakiwa wamesimama kimya
kwa dakikika moja kwa heshima ya mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir,
bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Hafidh alifariki dunia usiku wa
kuamkia leo mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa
Dimani, Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma
Novemba 11, 2016. Mbunge huyo alifariki dunia mjijini Dodoma usiku wa
kuamkia leo.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa
Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma
Novemba 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo
cha Mbunge wa Dimai Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11,
2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Kiongozi wa
Upinzania bungeni, Freeman Mbowe (kulia) wakishuhudia wakati mwili wa
mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir ukipandishwa kwenye ndege katika
uwanja wa ndege wa Dodoma ili kusafirishwe kwenda Zanzibar kwa mazishi
Novemba 11, 2016.
.............................................................................................
.............................................................................................
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa
Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir.
Bw.
Tahir amefariki saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa
Dodoma na mwili wake kuagwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kabla ya kusafirishwa
kwenda Zanzibar kwa mazishi.
Akizungumza
katika tukio hilo, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai, familia ya marehemu na wabunge wote.
“Tumepokea
taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Leo tupo katika wakati mgumu sana.
Tumeondokewa na viongozi wengi,” amesema.
Amesema
wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo. “Tumuombee marehemu, tuiombee familia iwe
na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.”
Bw.
Hafidh alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania
Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.
Enzi ya uhai wake, alishiriki kikamilifu katika masuala ya michezo; alikuwa
mwamuzi wa soka mwenye beji ya FIFA na kocha msaidiizi wa timu ya soka ya
Bunge.
Hadi
jana, Bw. Hafidh alishiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa
kupata viongozi wa Tawi la Umoja wa Wabunge WanaYanga mjini Dodoma ambapo yeye
alichaguliwa kuwa Katibu.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
S.
L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA,
NOVEMBA 11, 2016.








0 Comments