Random Posts

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA SPIKA MSTAAFU SAMWEL JOHN SITTA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta Ukiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.


Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta ukiwa katika eneo maalum mbele ya waombolezaji kwa ajili ya kufanyiwa idaba na tukio la utoaji heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimfariji Mama Margareth Sitta, Mjane wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Oktoba 11, 2016

 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko, pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli(Katikati), Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan(Mwenye shungi) Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa (wa mwisho kushoto) na Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif alli Idd (wa mwisho kulia) wakifuatilia idaba ya kuuaga Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta katika viwanja vya Karimjee kwa ajili.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi Mhe. Angela Kairuki akitoa salamu za serikali wakati wa shughuli ya utoaji heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwaeleza jambo Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif alli Idd(katikati) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho 
Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Oktoba 11, 2016
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisalimiana na waombolezaji wakati wa shughuli za utoaji heshima kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta.
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima  za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Oktoba 11, 2016
 Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Viongozi wastaafu wakiwapa pole ndugu na waombolezaji wakati wa shughuli za utoaji heshima kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta.
PICHA NA IKULU

Post a Comment

0 Comments