Jeneza lililobeba mwili wa Spika msaafu Samwel
Sitta likitelemshwa kutoka kwenye gari tayari kwa kupewa heshima na kupelekwa
nyumba ni kwake Masaki mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere leo Jijini Dar es Salaam.
Askari wakiwa wamebeba jeneza liliobeba mwili wa
aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Hayati, Samwel Sitta wakipita mbele ya Askari
maalum kwa ajili ya kutoa heshima na baadaye kupakia jeneza hilo tayari kwa
safari ya kuelekea nyumbani kwa marehemu leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Hassan Suluhu (kulia)
akimfariji mjane wa Spika msataafu wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Hayati. Samwel Sitt, Mhe. Margareth Simwanza Sitta (MB) mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndenge wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal I leo
jijini Dar es Salaam.
....................................................................................................
Na:
Frank Shija, MAELEZO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu amewaonga
watanzania katka mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la
Tanzania marehemu Samwel Sitta aliyefariki dunia saa 10.00 usiku wa kuamkia
tarehe 7 Novemba huko nchini Ujerumani alikokuwa kwa matibabu.
Mama
Samia aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa 8:
44 mchana akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali tayari kwa
kuupokea mwili wa marehemu Sitta uliowasili uwanjani hapo kwa usafiri wa ndege
ya Emirate majira ya saa 9: 05 Alasiri.
Viongozi
waliombatana na Mhe. Makamu wa Rais ni pamoja na Makamu wa Pili wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Idd, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na
Jumiya ya Afrika Mashariki Balozi Mahiga, Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na
Utawala Bora Mhe. Angerah Kahiruki, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
Wengine
ni Katibu Mkuu Kingozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda,na baadhi ya viongozi wa kiasiasa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM
Bara, Phillip Mangula, Msemaji wa Chama cha Mapinduzi Christopher Ole
Sendeka,aliyekuwa Mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Ragge, Mzee Pius Msekwa na
Profesa Ibrahim Aruna Lipumba wa CUF.
Akizungumza
wakati wa mapokezi hayo Waziri Mahiga alisema kuwa Taifa limepoteza kiongozi muhimu
ambaye alikuwa na mahusiano mazuri na watu wa makundi yote kitu kilichomfanya
kuwa mfano wa kuigwa.
Balozi
Mahiga aliongeza kuwa kitu muhimu ambacho viongozi tuapaswa kujifunza kutuka
kwake ni kuwa kiongozi siyo kipaji pekee bali ni ridhaa kutoka kwa watu kitu
ambacho ndicho kilimfanya Sitta kuwa kiongozi katika katika nafasi mbalimbali
za ungozi tokea Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne .
Aliongeza
kuwa ameacha funzo kuwa ili uwe kiongozi imara atupaswi kukata taama badala
yake unapaswa kusimamia misingi ya haki na ukweli ikibidi kutofautina na
wenzako kwa maslahi ya taifa.
Kwa
upande wake Msemaji wa CCM amemuelezea Sitta kama kiongozi aliyekuwa anahitaji
sana katika kipindi kwa kuwa alijipambanua kama mpambanaji wa adui rushwa na
ufisadi.
“
Tumempoteza mapambanaji muhimu has tukizingatia kuwa Serikali ya awamu hii
chini ya AMIRI Jeshi Mkuu Mhe. Rasi Dkt. Magufuli ipo katika vita kubwa dhidi
ya rushwa na ufisadi jambo ambalo Sitta alikuwa muumini wake” Alisema Ole
Sendeka.
Utaritibu
wa kuuga Mwili wa Marehemu Samweli Sitta zitaanzia na misaa ya shukrani
nyumbani kwake hapo kesho(leo) saa 1:30 asubuhi baadaye utawasili katika
viwanjwa vya Karimjee kwa ajili ya kuagwa kitaifa kuanzia 2;30 asubuhi kabla ya
kuelekea Dodoma ambapo wabunge watapata fursa ya kumuaga kasha utaelekea Urambo
moani Tabaro ambapo mazishi yake yanatarjiwa kufanyika huko siku ya Jumamsoi.
Bwan ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.



0 Comments