Random Posts

MATUKIO YA MAZISHI YA SPIKA MSTAAFU, SAMUEL SITTA, NOVEMBA 12, 2016 URAMBO

 Mjane wa Marehemu Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Mama Mzazi wa marehemu,  na watoto wa marehemu wakigusa jeneza na kushuhudia wakati mwili wa marehemu Samuel Sitta ulipoteremshwa kaburini katika mazishi yaliyofanyika urambo, Tabora, Novemba 12, 2016(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaina na Viongozi wa Serikali wa mkoa wa Tabora, Viongozi wa Vyama vya siasa na dini baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora akiwa njiani kwenda Urambo kwenye mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta Novemba 12, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora Novemba 12, 2016. Wote walikuwa wakienda Urambo kushiriki mazishi  ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora akieleke Urambo khudhuria mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta, Novemba 12, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu, Alex Malasusa  wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani katika mazishi ya Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta yaliyofanyika Urambo Novemba 12, 2016.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo bada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu, Spika Mstaafu Samuel Sitta, Urambo  mkoani Tabora ambako alishiriki mazishi Novemba 12, 2016.
  Maaskofu na wachungaji wakiuombea mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sitta kabla ya mazishi yaliyofanyia Urambo Tabora, Novemba 12, 2016.
 Bibi Kagoli Fundikira ambaye ni Mama Mzazi wa Spika Mstafu , marehemu Samuel Sitta akiongozwa kwenda kwenye kaburi la mwanae katika mazishi yaliyofanyika Urambo  Novemba 12, 2016

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mjane wa marehemu Spika Mstaafu,  Samuel Sitta baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu, Urambo Tabora kwa  mazishi Novemba 12, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Urambo mkoani Taboro Novemba 12, 2016.
  Bibi Kagoli Fundikira ambaye ni Mama Mzazi wa marehemu  Spika Mstaafu Samuel Sitta     akitupa udongo kwenye kaburi la mwanane katika mazishi yaliyofanyika Urambo, Tabora Novemba 12, 2016.
   Mama Margareth Sitta ambaye ni Mjane wa marehemu Spika mstaafu,  Samuel Sitta akitupa udongo kwenye kaburi la mumewe katika kazishi yaliyofanyika Urambo Novemba 12, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitupa udongo kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta katika mazishi  yaliyofanyika Urambo Novemba 12, 2016.
  Viongozi wa Vyama vya siasa na serikali pamoja na wanafamilia wakiweka udongo kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta katika mazishi yaliyofanyika Urambo, Novemba 12, 2016.
  Mjane wa Marehemu Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Mama Mzazi wa marehemu,  na watoto wa marehemu wakigusa jeneza na kushuhudia wakati mwili wa marehemu Samuel Sitta ulipoteremshwa kaburini katika mazishi yaliyofanyika urambo, Tabora, Novemba 12, 2016.
 Mama  Margareth Sitta ambaye ni mjane wa Spika Mstafu, marehemu Samuel Sitta akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe katika mazishi yaliyofanyika Urambo Novemba 12, 2016

  

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta katika mazishi yaliyofanyika Urambo Novemba 12, 2016.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akiweka shada la maua kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta katika mazishi yaliyofanyika Urambo, Novemba 12, 2016.
 Maaskofu  walioshiriki katika ibada ya mazishi ya Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta wakiweka shada la maua kwenye kaburi katika mazishi yaliyofanyika Urambo, Novemba 12, 2016

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Busega  na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Titus Kamani ambaye sasa ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Simiyu katika mazishi ya Spika Mstaafu Samuel Sitta yaliyofanyika Urambo Tabora, Novemba 12, 2016.  Kulia kwake ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kushoto kwake ni Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri

  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na baadhi  ya wanafamilia na ndugu wa marehemu Spika Mstaafu, Samuel Sitta bada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Urambo mkoani Tabora kwa mazishi Novemba 12, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na familia ya Spika Mstaafu marehemu Samuel Sitta baada ya mazishi yaliyofanyika Urambo Novemba 12, 2016.

Post a Comment

0 Comments