Hili ndilo
Daraja lililojengwa na wafadhili chini ya Bw. Hans Paul lina upana wa Mita 20,
uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani 3, urefu kwenda juu Mita 2.2 na
uwezo wa kudumu kwa miaka 50.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa akimkaribisha Vongozi wa
Serikali na wananchi wa Kata ya Engutoto kwenye uzinduzi wa daraja la Mto
Kijenge lililojengwa kwa ufadhili wa Dharam Singh Hanspaul
Diwani wa
Kata ya Engutoto kwa kupita Tiket ya Chadema
Mhe.Aman Reward alishirki katika
uzinduzi wa Daraja na kupongeza
Viongozi wa Mkoa na Jiji kwa namna wanavyowatumika wananchi
Diwani wa
Kata ya jirani ya Themi kupitia Tiketi ya Chadema Mhe. Melance Kinabo pia alishirki katika
uzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge.
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(kwanza kulia) akipokea Kero kutoka kwa mwananchi
kama zilivyowasilishwa na Mama Debora
wakati wa Unzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akizungumza
na wananchi wa Kata ya Engutoto na Moshono wakati wa Uzinduzi wa Daraja la Mto
Kijenge
Mkuu wa wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza
kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) na Bw. Bw. Jagjit Aggarwal
Daraja
walilokuwa wanatumia wananchi wa Engutoto na Moshono kabla ya kujengewa Daraja
la kiwango na Kampuni ya Dharam Sign Hanspaul
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizundua Daraja la Mto Kijenge
Wakazi wa
Kata za Engutoto na Moshono wakitoa shukrani zao kwa kukabidhi Mbuzi na kumvika
mavazi ya kimaasai Mfadhili aliwajengea
Daraja la Mto Kijenge Bw. Hans Paul.
...........................................................................................
Nteghenjwa Hosseah - Arusha
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka
Gambo amezinduzaa daraja la Mto Kijenge linalounganisha kata za Engutoto na
Moshono ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Dharam Singh Hanspaul.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amesema
daraja hilo ni ukombozi na msaada kwa wananchi wengi ambao walikua wakipata
adha kubwa ya kuvuka haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa kivuko cha uhakika
na kivuko kilichokuwepo awali kiliashiria
hali ya hatari kubwa kwa watoto, wazee, waendesha pikipiki, waenda kwa miguu
wote na zaidi hakuna Gari lililokuwa na uwezo wa kupita hapo.
Hii
ndio tunayoita kurudisha kwa jamii “Community
Social Responsibility”, kampuni hii ya Hanspaul imetoa msaada ambao utatoa
mchango mkubwa sana kwa jamii na sisi kama Serikali tunafarijika kwa kuona
wadau wanaunga mkono jitihada za Serikaili kwa kiwango hiki hili ni jambo la
kuigwa na Kampuni nyingine wajifunze katika hili.
Katika
uzinduzi wa daraja hili Rc Gambo
alitumia fursa hiyo alisikiliza kero za wananchi waliohudhuria na ambao wamelalamikia
uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya Serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo
ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani
katika kata ya Engutoto hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi
wapate huduma bora za ijamii.
Akiwasilisha
kero zake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bi. Zaituni Marunda amesema kuwa licha ya uuzaji holela wa ardhi kuna
migogoro ya ardhi katika kata hiyo na wananchi wengi wanaomiliki ardhi
bado hajapatiwa hati jambo ambalo linawapa wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa
na wawekezaji.
Aidha
Neema John aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu katika maeneo hayo wamekuwa
wakisumbuliwa na kero za maji, umeme na Zahanati hivyo wameiomba Serikali
iwasaidie kutatua kero hizo znazowaathiri zaidi kinamama ambao hutembea umbali
mrefu wakitafuta huduma za maji pamoja na kupata taabu wakati wa kujifungua.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi ripoti
ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia kero na
pia aliweza kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Kata kwa kuchangia Bati 100 na kuungwa mkono na Bw.
Hans Paul aliyetoa matofali 5000 huku Bw. Jagjit Aggarwal akichangia mifuko ya saruji 200 na Mkurugenzi
wa Jiji Bw. Athumani Kihamia kuahudi kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.
Daraja
la Mto kijenge lilioanza kujengwa mwezi Juni na kukamilika Agost 2016 lina
upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani tatu(3), urefu kwenda juu ni mita 2.2, uimara wa pekee na linaweza
kudumu kwa miaka 50; Ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 67 .










0 Comments