
Kamishna
Jenerali wa Mgereza – CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Wawekezaji wa masuala ya Kilimo cha kisasa mara baada
ya mazungumzo Ofisini kwake leo Novemba 2, 2016, Makao Makuu ya
Magereza(kulia) ni Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya
CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei(kushoto) ni Mwakilishi wa
Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi.
............................................................................................
Na; Lucas Mboje, Jeshi la Magereza – Dar es Salaam
KAMISHNA
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja amekutana na
Wawekezaji wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China pamoja na Kampuni ya
Wazawa ya KG CORPORATION na kumuahidi kushirikiana na Shirika la
Uzalishaji Mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) katika kuwekeza
katika miradi mbalimbali ya Kilimo cha kisasa, Madini na Viwanda
vinavyoendeshwa na Shirika hilo.
Akizungumza
na Wawekezaji hao leo asbuhi Ofisini kwake (Jumatano, Novemba 2, 2016)
alisema kwamba Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Uzalishaji
mali lina fursa nyingi za miradi ya uwekezaji kwenye sekta nyingi kama
vile Kilimo, Viwanda na Madini ambapo aliwahahakishia ushirikiano wa
kutosha kwenye uwekezaji wao
Wawekezaji
hao tayari wamefanya mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi ambapo wanatarajia kuiingia Makubaliano (MoU) na Jeshi la
Magereza kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimo cha kisasa
katika Gereza Idete lililopo Mkoani Morogoro pamoja na Mradi wa Ngo’mbe
wa nyama Gereza Ubena, Mkoani Pwani.
Kwa
upande wake Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya CAMCE
kutoka nchini China Bw. Lane Lei alisema amefurahishwa na ziara
waliyofanya nchini na wapo tayari kuwekeza hapa Tanzania.
Naye,
Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi ambayo
inashughulikia na masuala ya Kilimo cha mazao ya chakula na nyama
alisema watawekeza kwenye kilimo hususan cha umwagiliaji na watajenga
Kiwanda kwa ajili ya usindikaji.
Shirika
la Uzalishaji mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) lina jumla ya
Miradi 23, kati ya hiyo miradi 15 ni ya kilimo na mifugo na 8 ni ya
viwanda vidogo vidogo, pia zipo shughuli za mradi wa Kikosi cha Ujenzi
zinazosimamiwa na Shirika hilo.
Mkakati
wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali
pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ikiwemo uwekezaji wa ubia kwenye
miradi yake ili kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa katika
utekelezaji wa majukumu yake.
0 Comments