Na.Alex Mathias.
.....................
Kikosi
cha Simba kimetua jijini Mbeya kwa kazi moja kuchukua alama tatu muhimu
dhidi ya wenyeji Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine mchezo wa
Ligi Kuu Tanzania bara kufunga pazia la mzunguko wa kwanza.
Akizungumza
kutoka Mbeya Meneja wa Simba,Mussa Hassani Mgosi amesema kuwa
wanamshukuru Mungu kwa kufika salama tayari kwa mpambano huu wa kesho na
mchezo huo utakuwa mgumu ila tumejipanga kupata ushindi na kuchukua
alama tatu muhimu na pia tutawakosa wachezaji wetu watu kutokana sababu
mbalimbali.
"Ni kweli tutawakosa Ibrahimu Ajibu kafiwa na mtoto
wake baada ya Mke wake kujifungua na bahati mbaya mtoto alikufa,Abd
Banda pamoja na Ame Ali nao hatukuondoka nao kutokana na sababu
mbalimbali na wengine waliobaki tuko nao na kesho tunaingia kwa hasira
kubwa mno hii ni baada ya kupokea mchezo wetu na African Lyon"alisema
Mgosi
Aidha Mgosi amewaomba mashabiki wa Simba pamoja na
wanachama kuendelea kushikamana kwa umoja wao na kuwatoa hofu kuwa kesho
wataibuka na ushindi kama kawaida japo ni mechi ngumu kwao licha ya
kufungwa wekundu wa msimbazi bado wapo kileleni wakiwa na alama 35.
Kwa
upande wa Prisons kupitia msemaji wao Enock Mwanguku,amesema kuwa
wanaiheshimu Simba kwa kuwa ni kongwe ila wao wapo tayari kuwafunga na
kuweza kuchukua alama tatu kamwe hatuwezi kupoteza mara mbili katika
uwanja wetu wa nyumbani.
"Sisi tumejeruhiwa kwa kufungwa na
Yanga hivyo tunawaonya Simba wasitengemee mteremko kwa kuja kuchukua
alama tatu kiukweli tumejipanga na tutashinda Simba wanatujua
tunapokutana nao jasho huwa linawatoka"alisema Mwanguku

0 Comments