Hafidh Ally Tahir (enzi za uhai wake)
........................................
Mhe Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tannzaia anasikitika
kuwatangazia kuwa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar Mheshimiwa
Hafidh Ali Tahir amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo katika Hospitali ya
General hapa Dodoma.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu
zitatolewa hapo baadae. Mhe Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza
msiba huu.
Awali Marehemu pia alikuwa mwalimu wa
soka kwenye timu ya Bunge Sports Club na mpaka usiku wa Novemba 10 alikuwa
pamoja na waheshimiwa wabunge katika vikao
mpaka saa 2.45 usiku

0 Comments