JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA
MAKAZI
TANZIA
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi anasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi wa
Wizara Bwana Elvis Nyambita Magare, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ramani Idara
ya Upimaji na Ramani kilichotokea tarehe 11/11/2016 Nyumbani kwake mtaa Mindu
Upanga Jijini Dar es salaam. Ratiba ya kuaga Mwili wa Marehemu ni leo tarehe
14/11/2016 saa 4:00 Asubuhi hadi 7:00 Mchana na Kusafirishwa. Mazishi yatafanyika
siku ya Jumatano tarehe 16/11/2016 Kijiji cha Shirati Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.


0 Comments