Baraza la
Wauguzi na Wajunga nchini wametakiwa kutowaonea aibu wale wote
wanaoanzisha vyuo vya afya kama mradi wa kujiingizia fedha bila ya kuwa
na taaluma hiyo kwani kunapelekea kuhatarisha Maisha na afya za
watanzania.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la
kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo mjini
kibaha Pwani.
“Hatusemi
wasianzishe vyuo,bali vyuo vyote viwe vyenye hadhi ya kutoa wataalam
stahili ,visajiliwe na vikaguliwe mara kwa mara ili vizalishe wauguzi
wenye sifa na ujuzi stahili,uuguzi siyo ujasiliamali,hakikisheni
mnavifungia vyuo vyote feki ili tuweze kudhibiti utitiri huu” alisema
Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy alisema hivi sasa kumekuwepo na utitiri wa vyuo vingi vya
uuguzi ambavyo havijasajiliwa na havizalishi wauguzi ambao wanastahili
kuajiriwa kwenye sekta ya afya na hivyo kuhakikisha wanasimamia taaluma
hiyo na kuvifungia mara moja vyuo vilivyokosa sifa.
Waziri
Ummy alisema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa
unaofanywa na wauguzi katika hospitali zote nchini hivyo maboresho
yatafanyika na kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi kwa wauguzi.
“Asilimia
80 za kazi zote katika hospitali zetu nchini zinafanywa na wauguzi na
wakunga hivyo Serikali imesikia kilio chenu na tutahakikisha tatizo hili
tunalitatua” alisema Ummy.
Hata hivyo Waziri Ummy aliwataka wauguzi kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia maadili na viapo vyao vya kitaaluma kwa maendeleo ya Afya nchini.
Kwa upande wa Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini Bi. Lena Mfalila alisema jengo hilo linajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza limegharimu pesa ya kitanzania shilingi bilioni 2.2.
Aidha
Bi. Mfalila alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho ulianza Desemba 2015 kwa
awamu ya kwanza na kiinatarajiwa kukamililika na kuanza matumizi yake
Januari2017 .
0 Comments