Waogeaji na
viongozi wa Dar Swim Club wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na kikombe,
medali walizoshinda katika mashindano ya Taifa ya Kenya yajulikanayo kwa jina
la Kenya National’s Age groups open and relay swimming championship. DSC
ilishinda jumla ya medali tisa katika mashidano hayo.
Kocha wa
timu ya kuogelea ya Dar Swim Club (DSC), Salum Mapunda (kushoto) akiwa na
waogleaji wake kabla ya kushindana katika mashindano ya Taifa ya Kenya
yajulikanayo kwa jina la Kenya National’s Age groups open and relay swimming
championship. DSC ilishinda jumla ya medali tisa katika mashidano hayo.
Kocha wa timu ya kuogelea ya Dar Swim Club
(DSC), Salum Mapunda akiwaelekeza waogeaji wake wakati wa mashindano ya Taifa
ya Kenya yajulikanayo kwa jina la Kenya National’s Age groups open and relay
swimming championship. DSC ilishinda jumla ya medali tisa katika mashidano.
...................................................................................................
Na Mwandishi
wetu
Klabu ya
mchezo wa kuogelea ya Dar Swim Club (DSC) imefanya vizuri katika mashindano ya
wazi nay a umri ya Kenya baada ya kutwaa
medali tisa, kikombe na vyeti.
Mashindano
hayo ya wazi yalifanyika mjini Mombasa na kushirikisha timu kutoka mataifa
mbalimbali ikiwemo, Uganda, Kenya, Swaziland na Tanzania Bara.
Mbali ya DSC, klabu ya Shule ya Kimataifa ya
Moshi (ISM) nayo ilishiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Aga
Khan Academy.
Katibu Mkuu
wa DSC, Inviolata Itatiro alisema kuwa mwogeleaji wake, Marin de Villard aliweze kutwaa medali saba na vyeti tisa kwa
kufanya vizuri katika staili mbalimbali.
Marin
alishinda medali ya dhahabu katika staili ya freestyle ya mita 50 na 100 na
baadaye kushinda medali ya fedha katika staili ya backstroke kwa mita 50 na 100
kwa waogeleaji wa kati ya miaka 10 na 11.
Inviolata
alisema kuwa Marin pia alishinda medali ya shaba kwa mita 100 na 200 katika
staili ya Medley (IM) na vile vile kushinda mdali ya shaba katika staili ya butterfly
kwa mita 100.
Muogeleaji
mwingine, Celina Itatiro aliweza kushinda medali mbili na vyeti nane kwa
kufanya vizuri. Celina alishinda medali za sahaba katika staili za freestyle na
butterfly katika mashindano ya mita 100.
Naye Chichi
Zengeni alifanya vyema na kutambuliwa kwa kupewa vyeti vinne huku akihimarisha
muda wake wa kuogelea mara 10, huku Kayla Temba akihimarisha muda wake mara
nane), Reuben Monyo akihimarisha muda wake mara tano na Peter Itatiro
akihimarisha muda wake mara tano.
“Tumejivunia
sana matokeo haya, ni mazuri kwani waogeleaji wetu wengi wameshiriki mara ya
kwanza mashidano ya kimataifa, tunachoangalia sisi ni jinsi gani muogeleaji
wetu anahimarisha muda wake, kupata uzoefu na kushinda,” alisema Inviolata.
Inviolata
alisema kuwa klabu yao imedhamiria kushiriki katika mashindano mengi zaidi ya
nchini na Kimataifa ili kujenga uwezo wa waogeleaji wake wachanga kwa ajili ya
mashindano makubwa ya kimataifa kama Mataifa ya Afrika (All Africa Games),
Jumuiya ya Madola, Olimpiki na Mashindano ya Dunia



0 Comments