
Wachezaji wa timu ya Mbeya Citywakishangilia goli.
…………………………………………………….....................................................
Na.Alex Mathias.
Mabingwa watetezi Yanga wameangukia pua baada ya kukubali
kichapo cha mabao 2-1 toka kwa wenyeji timu ya Mbeya City mchezo wa Ligi
Kuu Tanzania bara huu ni ushindi wa kwanza kwa Mbeya City tangu wapanda
Ligi.
City walikuwa wa kwanza kupata bao likifungwa na Hassan
Mwasapili baada ya kupiga faulo iliyoenda moja kwa moja na kumshinda
Mlinda mlango Dida licha ya kuongoza City waliendelea kulishambulia
lango la wageni kama nyuki.
Kenny Ali alipeleka kilio kwa mashabiki wa Yanga ambao
walikuwa wamefurika uwanjani hapo dakika ya 36 hata hivyo kuingia kwa
bao hilo kulileta mzozo mkubwa kwa mwamuzi akizongwa na wachezaji hali
ambayo ilipelekea mwamuzi kulikataa bao na baadaye alikubali na mchezo
kuendelea.
Dakika ya 45 Donaldo Ngoma aliifungia Yanga bap la kufutia
machozi baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Msuva na hadi mapumziko
City walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko kwa
kuwatoa Mbuyu Twitte,Amis Tambwe na Deus Kaseke na kuwaingiza Geofrey
Mwashiuya,Obrey Chirwa na Thabani Kamusoko hata hivyo mabadiliko hayo
hayakuzaa matunda kwa mabingwa hao watetezi.
Dakika ya 80 Betra Nchimbi nusura
afunge bao la tatu kwa City baada ya kuwachambua mabeki pamoja na
Golikipa na shuti lake lilitoka nje hadi mwamuzi anamaliza mpira Mbeya
City wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuandika rekodi ya kwanza
kuwafunga Yanga.
0 Comments