African Lyon imeendelea kuvipa
shida vigogo vya VPL, baada ya Yanga kutoka nyuma kusawazisha goli na
kuambulia pointi moja katika matokeo ya 1-1.
Lyon walitangulia kupata bao kupitia kwa Ludovick lakini Tambwe alisawazisha bao hilo kuiokoa timu yake isipoteze mchezo
Bado Yanga wamekuwa wababe mbele
ya Lyon kwa sababu katika michezo nane iliyopia Lyon hawajafanikiwa
kutoka na ushindi, wamepata sare mbili sawa na pointi mbili huku Yanga
wao wakiwa wameshinda mara sita na sare mbili na kupata pointi 20 dhidi
ya Lyon.
Mchezo uliopita uliochezwa August
28 mwaka huu, Yanga iliifunga Lyon 3-0 magoli yakifungwa na Deus Kaseke,
Simon Msuva na Juma Mahadhi.
Lyon imekuwa tishio kwa vigogo
kwasababu iliweza kuizuia Azam katika mchezo wa ufunguzi wa msimu huu
2016/17 na kutoka sare ya kufungana bao 1-1 huku Azam wakitoka nyuma na
kusawazisha.
Simba walijikuta wakichezea
kichapo cha goli 1-0 November 6 mwaka huu mchezo uliochezwa kwenye
uwanja wa Uhuru ikiwa ni raundi ya kwanza ya msimu huu.
Lyon wakawabana tena Azam katika
mchezo wa marudiano raundi ya pili ya ligi na kutoka suluhu December 18,
2016 kabla ya Yanga kulazimisha sare katika mchezo wa leo December 23.
African Lyon imefanikiwa kupata
pointi 6 dhidi ya Yanga, Simba na Azam. Tayari imesha cheza mechi mbili
na Azam na Yanga huku ikisubiri mechi moja ya marudiano dhidi ya Simba.
Yanga inaendelea kusalia katika
nafasi ya pili ikiwa na pointi zake 37 pointi moja nyuma ya Simba ambayo
itacheza kesho December 24 dhidi ya JKT Ruvu.
Endapo Simba itashinda mchezo huo
itaongeza gape la pointi hadi kuwa nne kwa sababu itakuwa imefikisha
pointi 41 huku Yanga ikiwa na pointi 37, lakini kama Simba itafungwa
bado itaendelea kuongoza kwa pointi moja wakati ikitoka sare itakuwa
kileleni kwa pointi mbili.

0 Comments