Maofisa
Waandamizi wa Masoko na Mauzo wa TBL Group wakionyesha kinywaji cha
Chibuku Super katika chupa mpya wakati wa hafla ya uzinduzi jijini
Mwanza.
.......................................................................................................
Kampuni ya
TBL Group imezindua Chibuku Super kwenye chupa ya bia ya
glasi yenye ujazo wa ML500, chupa hii ni nzuri na ya kuvutia ya glasi inayorudishwa
(Returnable) ina ujazo wa nusu lita na
itauzwa kwa bei ya shilingi 700/- tu, kwa chupa.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika
ukumbi wa kiwanda kilichopo eneo la Pasiansi Mwanza , Meneja Masoko wa TBL
Group, Bw. Oscar Shelukindo; alisema “leo ni siku ya furaha kubwa sana kwetu TBL
na kwa watumiaji wote wa Bia yetu hi ya asili , kwani tumeweza kuzindua Bia hii
ya “Chibuku Super” kwenye chupa ya glasi ambayo inatarajiwa kuleta mapinduzi
makubwa katika soko la Bia hapa nchini. Bia hii imetengenezwa kwa utaalamu wa
hali ya juu na kwa kutumia mitambo ya kisasa kabisa, hivyo kuwahakikishia
wanywaji Ubora wa hali ya juu”
Shelukindo alisema, Bia hii inatengenezwa kwa
kutumia malighafi za hapa nyumbani, ikiwemo nafaka ya mahindi na mtama bora
toka kwenye ardhi yetu, haya yote yanatupa kila sababu sisi watanzania kujivunia
kilicho chetu na kukumbuka asili yetu, kwani hii ni Bia yetu ya asili. Chibuku
Super ina kilevi cha asilimia 4, kinachokufanya uweze kuitumia kwa muda mrefu ukiwa
na marafiki, lakini pia inakupa lishe nzuri kutokana na virutubisho
vinavyopatikana katika nafaka zinazotumika kutengeneza bia hii.
Akizungumzia
juu ya usambazaji wa Bia hii, meneja mauzo wa TBL Bw. Fred Kazindogo amesema;
Baada ya uzinduzi huu unaofanyika leo, Bia hii ya Chibuku Super kwenye chupa ya
ML 500 NA KWA BEI YA 700/-TU itaanza kupatikana kesho kwa wasambazaji wakubwa
na katika baa mbliimbali na sehemu
nyinginezo zinazouza vileo. “Tunatarajia
wateja na wapenzi wa bia wataifurahia bia hii mpya itakayouzwa kwa bei ya
shilingi 700/- tu kwa chupa. Kreti itauzwa kwa 14,000/- kwa wasambazaji”
Alisema kwa
sasa Bia hii itaanza kupatikana katika mikoa 15 ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Geita,
Tabora, Singida, Kigoma, Simiyu, manyara , Kilimanjaro, Arusha, Katavi, Mbeya na Rukwa.
Na kwa
wauzaji wa jumla, tunatarajia watahamasika kuuza bia ya Chibuku Super kwani ina
faida nzuri na bia hii inadumu kwa miezi 4 kwenye soko ambao ni mrefu sana
kulinganisha na products zetu nyingine, alisema Kazindogo
“Tuna imani kubwa wapenzi wa Bia wataipokea
Chupa hii mpya kwa kwa bei ya 700/- kwa Shangwe na furaha kubwa, na pia
watatumia Bia hii kuonyesha kuwa wanajali Asili yao”. Alisema Kazindogo.

0 Comments