Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt.
Abdallah Possi akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee
(wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake katika shule ya Masasi yenye kuhudumia
wenye ulemavu Mkoani Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt.
Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) akiwa katika ziara ya kuangalia maeneo ya
shule ya Masasi inayohudumia wanafunzi wa mahitaji maalum wakati wa ziara yake
mkoani Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt.
Abdallah Possi akikagua moja ya bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum la Shule
ya Masasi Mkoani Mtwara
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt.
Abdallah Possi akionesha namna ya kutumia Kurunzi ya mwanga wa jua kwa baadhi
ya wazee wenye ukoma wanaoishi katika Kambi ya Mkaseka Wilaya ya Masasi Mkoani
Mtwara na kuwapatia wazee hao kurunzi 20 kwa kila nyumba.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Halima Dendego akimweleza Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi
historia fupi ya mkoa huo wakati wa ziara yake mkoani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt.
Abdallah Possi (wa sita kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara mara bada ya
kumaliza ziara yake mkoani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt.
Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari katika ziara yake
alipotembelea Shule na Makazi ya wazee Wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
...............................................................................................................
Na. Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu,
Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameitaka jamii kuzingatia haki na usawa kwa watu wenye
ulemavu nakuondokana na imani
potofu za kuona watu wenye ulemavu hawana uwezo wa kufanya shughuli za
maendeleo.
Mhe. Possi ameyasema hayo kwa nyakati tofauti
alipotembelea Vituo na Shule zinazohudumia watu wenye mahitaji maalum vya
Nandanga, Rasi Bula, Shule ya msingi Nyangao mkoani Lindi pamoja na makazi ya
wenye ulemavu na Ukoma ya Mkaseka, Chuo cha wenye Ulemavu cha Mtapika, shule ya
Lulindi na Masasi mkoani Mtwara.
Katika ziara hiyo Mhe.Possi alisisitiza jamii zibadili mitazamo hasi juu
ya masuala ya haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha katika
shughuli zote na kuwapa vipaumbele vya fursa sawa.
“Ninasisitiza jamii ibadili mitazamo
dhaifu juu ya haki na usawa wa kuwashirikisha watu wenye ulemavu kwani wana
uwezo wa uzalishaji endapo tutawapa fursa sawa kama ilivyokuwa kwa wakina mama
walipoachwa nyuma muda mrefu ila jamii imeona fursa ndani yao, iwe hivyo hivyo
kwa watu wenye ulemavu” alisema.
Aidha Waziri Possi ameweka mkazo juu ya
kuwahusisha na kutokuwaona kuwa ni kundi la kuachwa nyuma na kama tegemezi.
“sheria
zipo wazi kabisa zinazotuelekeza juu ya haki na usawa kwa watu wenye ulemavu
kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya watu wenye Ulemavu namba 9 ya mwaka 2010
inayoeleza haki za watu wenye Ulemavu kuwahudumia kwa haki na usawa na
kuboresha maeneo muhimu ikiwemo fursa za kielimu, ajira, kiuchumi na kijamii,”
alieleza.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa
Mhe. Joseph Mkirikiti alikiri kuyapokea yote aliyoeleza Mhe.Waziri katika ziara
yake na kuipongeza Serikali kwa juhudi za kuisaidia jamii bila kujali hali zao
na tofauti zao.
“Ninaipongeza
Serikali ya Awamu ya Tano inayowajali wanyonge na kujali haki zao pamoja na
mhe. Waziri kwa kuona umuhimu wa kututembelea wana Ruangwa na tunaahidi
kukuweka katika kumbukumbu zetu maana umewagusa wakazi wa Mtwara hususani wazee
na watu wenye ulemavu.”Alisisitiza Mkuu wa Wilaya hiyo.
Nae Afisa Mfawidhi kituo cha Kulelea wazee
wenye ukoma cha Mkaseka Bw. Cleophace Nguli aliiomba Serikali kuendelea
kuwakumbuka watu wenye ulemavu ikiwa ni watu waliosahaurika na kuendelea
kupongeza hatua zilizopo kwa sasa.







0 Comments