Wanafunzi wa Elimu ya Awali ambao wamehitimu
wakisoma risala kwa Mgeni Rasmi Diwani
wa Kata ya Segerea jijini Dar es salaam Edwin Mwakatobe pamoja na wazazi (hawapo
pichani) wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali
katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam.
Diwani wa Kata ya Segerea jijini Dar es salaam
Edwin Mwakatobe akitoa hotuba wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi
wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa
wiki jijini Dar es salaam.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Shule shule ya Awali na
Msingi ya Genius Kings Bw. Julius Rutabanja akitoa hotuba wakati wa siku ya
wazazi na mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali
na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Awali na Msingi
ya Genius Kings Machange Kisyeri akitoa neno la shukrani mara baada ya Mgeni
Rasmi na Diwani wa Kata ya Segerea jijini Dar es salaam Edwin Mwakatobe (hayupo
pichani) mara baada ya kutoa hotuba wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya
kuwaaga wanafunzi wa elimu ya awali katika hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aloyce Siame shule ya
Awali na Msingi ya Genius Kings akitoa taarifa ya shule wakati wa siku ya
wazazi na mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali
na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa Elimu ya Awali ambao wamehitimu
wakisoma risala kwa Mgeni Rasmi Diwani
wa Kata ya Segerea jijini Dar es salaam Edwin Mwakatobe pamoja na wazazi (hawapo
pichani) wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali
katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam.
Wanafunzi wa shule ya Awali na Msingi ya Genius
Kings wakionesha umahiri wao katika michezo wakati wa siku ya wazazi na
mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya
Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya Awali na
Msingi ya Genius Kings Jackson Nziku akionesha wageni pamoja na wazazi jaribio
la namna ya kuchuja maji machafu kwa matumizi ya kawaida wakati wa siku ya wazazi
na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya
Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Aliyevaa suti na tai
nyekundu ni Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo Machange Kisyeri.
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya Awali na
Msingi ya Genius Kings Irene Valentino akionesha wageni pamoja na wazazi
jaribio la namna ya uoteshaji wa mbegu na umuhimu wa maji, mwanga na hewa wakati
wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya
Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wazazi wakifuatilia michezo wakati wa siku
ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na
Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa elimu ya awali wakati wa siku ya wazazi
na mahafali yao katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa
wiki jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi na Diwani
wa Kata ya Segerea jijini Dar es salaam Edwin Mwakatobe (aliyevaa skafu) akiwa
katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na walimu walimu wa shule ya Awali na
Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri
Mangi)
.........................................................................
Na Eleuteri Mangi
Wazazi na walezi wametakiwa
kusimamia watoto wao ili kuhakikisha wanapata elimu stahiki wakati wote
wanapokuwa shuleni hatua ambayo itawasadia maisha yao na kupata viongozi wazalendo
kwa nchi yao.
Kauli hiyo imetolewa na
Diwani wa Kata ya Segerea Edwin Mwakatobe mwishoni mwa wiki wakati wa siku ya
wazazi na mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali
na Msingi ya Genius Kings jijini Dar es salaam.
“Tuwasimamie watoto
tusiwakatie tamaa, wasiposimamiwa vizuri sasa wakiwa katika umri wa masomo,
tutawapoteza na hivyo kuharibu maisha yao ya baadae, hii ni rasilimali kwa
familia na kwa taifa” alisema Diwani Mwakatobe.
Katika kuhakikisha
shule inatoa elimu yenye tija kwa wanafunzi na wazazi, Diwani Mwakatobe alisema
kuwa amefurahishwa na shule ya Genius Kings kuitikia wito wa Serikali kwa
wawekezaji binafsi ndani ya nchi kuchangia jitihada za kuendeleza sekta ya
elimu nchini.
Ili kuhakikisha
mafanikio katika sekta ya elimu yanakuwa endelevu na Watanzania wengi
wananufaika na jitihada za wawekezaji binafsi, Diwani Mwakatobe alisema kuwa ni
lazima kila mdau wa elimu atimize wajibu wake kikamilifu ikiwemo kuendesha
shule kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi zilizowekwa.
Akimkaribisha Mgeni
Rasmi, mmoja wa Wakurugenzi wa Shule hiyo Bw. Julius Rutabanja alinukuu maneno ya maandiko
Matakatifu kutoka Mithali 22:6, yanayosema “Mlee mtoto katika njia impasayo
kuienenda, naye hataiacha hadi uzeeni mwake”.
Bw Rutabanja aliongeza
kuwa msingi mkubwa wa shule yao sio tu kutoa elimu bora, kuinua kiwango cha
elimu nchini na kuibua vipaji vya watoto, bali ni pamoja na kuhakikisha watoto hao
wanapata malezi ya kimwili, kiroho na kimaadili.
Awali akitoa taarifa
ya shule kwa Mgeni Rasmi na wageni waalikwa, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aloyce
Siame alisema kuwa tangu kuanzishwa shule hiyo Januari 7, 2008 imekuwa na
mafanikio makubwa katika kutoa taaluma bora kwa ongezeko kubwa la ufaulu wa
wanafunzi wa darasa la saba katika mitihani ya taifa.
Mwal. Siame amewadhihirishia
wazazi na walezi pamoja na wageni waalikuwa kuwa ufaulu wa wanafunzi katika
shule hiyo umekuwa mara zote uwe wa alama “A”, ufaulu huo mara zote umekuwa
ndio dira yao kwa kuhakikisha wanapunguza ufaulu wa alama “B” na ikiwezekana usiwepo ufaulu wa alama “C”
na “D”.
Katika matokeo ya
mwaka 2016, Mwalimu Mkuu huyo alisema kuwa wanafunzi wa darasa la saba
waliofanya mtihani wa kitaifa wamefaulu vizuri ambapo shule hiyo imekuwa ya nne
kiwilaya, ya 17 kimkoa na y a 53 kitaifa kati ya shule 8,109.
Akionyesha mtiririko
wa ufaulu mwalimu Siame alisema kuwa
mwaka 2013 shule hiyo ilikuwa na watahiniwa 32 wanafunzi wane tu ndio walipata
alama “A”, mwaka 2014 kulikuwa na watahiniwa 49, wanafunzi 20 walipata alama
“A”, mwaka 2015 kulikuwa na watahiniwa 57, wanafunzi 40 walipata alama “A” na
mwaka 2016 kulikuwa na watahiniwa 65, wanafunzi 49 walipata alama “A” na
wanafunzi 16 walipata alama “B” wakati hakuna mwanafunzi aliyepata alama “C) na
“D”.
Mafanikio hayo yanatokana
na ushirikiano mzuri kati ya wanafunzi, wazazi na uongozi wa shule kwa
kuwapatia wanafunzi malezi na usimamizi mzuri bora hatua ambayo ndio imekuwa
kichocheo cha ufaulu huo.
















0 Comments