Na Jonas Kamaleki, Paris.
Manispaa
ya Uijiji Kigoma imeazimia kuwashirikisha wananchi wake katika mipango ya
maendeleo na kubadli utamaduni uliokuwepo wa kuitegemea Serikali kuwaletea
mipango yake.
Hayo
yamesemwa jana Jijini Paris na Mratibu
wa Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) Kigoma, Mhandisi Sultan
Ndaliwo wakati wa kufunga Mkutano wa Kilele wa mpango huo OGP.
Mhandisi
Ndaliwo amesema ushirikishwaji huo utasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza
kwa wananchi bila kuwepo kwa ukiritimba kwani masuala hayo yatakuwa
yanajulikana wazi kwa wananchi.
"Nimefurahishwa
na jinsi jiji la Paris linavyowashirikisha wananchi wake katika kupata
maendeleo yao jambo ambalo tutaenda kulitumia Kigoma," alisema Ndaliwo.
Ameongeza
kuwa anaamini Kigoma Ujiji inakwenda kubadilika kutokana na utekelezaji wa
Mpango Mkakati waliojiwekea unatekelzwa ipasavyo.
Kwa
upande wake, Meya wa Manispaa ya Ujiji Kigoma, Sultani Hussein Luhavi amesema
ataenda kuweka mfumo wa utoaji taarifa kwa haraka ambapo kunatokea tatizo
katika eneo lolote ndani ya Manispaa ili lifanyiwe kazi na wahusika (tracking
system).
Amezishauri
Manispaa nyingine zijenge utamaduni wa kuwasilkiliza wananchi na kuwashirikisha
ipasavyo katika mipango ya maendeleo.
"Utendaji
wa jinsi hii utabadilisha Manispaa yetu na kuifanya ipige hatua kubwa katika
maendeleo," alisema Luhavi.
Luhavi
amezitaka Manispaa na Halmashauri za Miji nchini kuiga mfano wa Manispaa ya
Ujiji Kigoma ili kuharakisha maendeleo yao.
Halmashauri
ya Manispaa ya Ujiji Kigoma ni Kati ya Manispaa 15 duniani zilizojiunga na OGP
kama manispaa na si nchi.
Manispaa
nyingine zilizojiunga na Mpango huo ni pamoja na Austin ya Marekani;
Bojonegoro, Indonesia; Buenos Aires, Argentina; Elgeyo Marakwet, Kenya;
Jalisco, Mexico; La Libertad, Peru; Madrid, Spain; Ontario, Canada; Paris,
France; Sao Paulo, Brazili; Scotland, Uingereza; Sekondi-Takoradi, Ghana;
Seoul, Korea Kusini and Tbilisi, Georgia.
0 Comments