Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni akimkabidhi Kitambulisho cha Taifa cha Wageni, Leonie Schollmeyer
(kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar leo. Masauni licha ya kupewa
elimu kuhusiana na utendaji wa kazi wa ofisi hiyo, pia alizungumza na watumishi
wa Mamlaka hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa weledi kwa kuwahudumia wananchi
ili kuiletea mamlaka hiyo mafanikio zaidi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akifanya
usafi na wanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Miembeni katika Hospitali ya
Mnazi Mmoja Zanzibar. Masauni alialikwa na Baraza hilo kushiriki kufanya usafi
nao na baadaye aliwatembelea wagonjwa wa hospitali hiyo akiwa na Naibu Spika wa
Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma (hayupo pichani) pamoja na Mkuu wa
Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas (hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni akizungumza na Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),
Zanzibar wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi ya kujifunza shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Masauni licha ya kupewa elimu
kuhusiana na utendaji wa kazi wa ofisi hiyo, pia alizungumza na watumishi wa
Mamlaka hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa weledi kwa kuwahudumia wananchi ili
kuiletea mamlaka hiyo mafanikio zaidi. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka
hiyo, Zanzibar, Hassan Haji Hassan.
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan
Juma (kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) wakimsikiliza Nesi
Msaidizi Mkuu wa Wodi ya Upasuaji wa Uti wa Mgongo na Kichwa katika Hopsitali
ya Mnazi Mmoja, Hadia Mmadi, wakati alipokuwa anawafafanulia kuhusu wagonjwa
wanavyopasuliwa. Viongozi hao walifanya ziara katika eneo hilo, mara baada ya
kufanya usafi mazingira mbalimbali ya hospitalini hapo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (watatu kushoto mstari wa mbele), Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar, Hassan Haji Hassan (watatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa
Mamlaka hiyo, mara baada ya Masauni kumaliza ziara yake ya kikazi kuitembelea
Mamlaka hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia)
akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya
Miembeni, Kikwajuni, Zanzibar, mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika
maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Mnazi Mmoja. Vijana hao walimwalika Mbunge
wao ili wajumuike naye katika kuweka safi zaidi mazingira ya Hospitali hiyo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 Comments