Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kaunda suti) akitoka ndani ya Kituo cha Polisi
cha Bububu, Unguja, Zanzibar mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni
hapo leo. Naibu Waziri huyo alitoa agizo kwa Kamishna Hamdan Omar Makame (hayupo
pichani) kuwaondoa haraka wamiliki wa miradi mbalimbali iliyopo eneo la Kituo hicho
pamoja na katika maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo, Zanzibar.
Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni akizungumza na Maafisa wa Polisi na Askari wa Usalama Barabarani katika
Ukumbi wa Jeshi la Polisi wa Bomani, Drill Shed, Unguja, Zanzibar. Masauni
alilitaka Jeshi hilo, kuwakamata madereva wa magari pamoja na pikipiki wanaovunja
sheria za usalama barabarani pamoja na kuwachukulia hatua kali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Omar Makame
pamoja na Watendaji wengine wa Jeshi hilo, wahakikishe wanawaondoa wamiliki
wote wa miradi binafsi katika eneo la Jeshi kwa kuanzia na Kituo cha Polisi
Bububu. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akionyeshwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi
cha Bububu, Abdulhalim Ali Haji, mpaka wa Kituo cha Polisi cha Bububu, Unguja,
Zanzibar, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo.
Masauni alipiga marufuku miradi binafsi iliyozunguka kituo hicho.
Mkuu wa Trafiki Wilaya ya Mjini, Unguja,
Zanzibar, Mohamed Talihata, akimuuliza swali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati kiongozi huyo alipofanya mazungumzo
na Maafisa wa Polisi na Askari wa Usalama Barabarani katika Ukumbi wa Bomani,
Drill Shed, Unguja. Masauni alilitaka Jeshi hilo, kuwakamata madereva wa magari
pamoja na pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani pamoja na
kuwachukulia hatua kali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamishna wa Polisi Zanzibar,
Hamdan Omar Makame alipokuwa anatoa taarifa ya Utendaji wa Jeshi la Polisi
Zanzibar katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo, Zanzibar. Masauni
alilitaka Jeshi hilo liweke mikakati imara ya kupambana unyanyasaji wa kijinsia
ambao umeshika kasi Zanzibar. Naibu Waziri huyo pia alifanya ziara ya
kushtukiza katika Kituo cha Polisi cha Bububu na alitoa maelekezo kwa uongozi
wa Jeshi hilo, kuhakikisha wanaondoa miradi binafsi iliyopo katika eneo la
Kituo hicho.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza
Kamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani, Zanzibar, Kamishna Msaidizi,
Mkadam Khamis alipokuwa anatoa taarifa ya Usalama Barabarani katika kikao
kilichowashirikisha Maafisa wa Jeshi hilo pamoja na Askari wa Usalama
Barabarani, kilichofanyika katika Ukumbi wa Bomani, Drill Shed, Zanzibar.
Masauni aliwataka askari hao kuwakamata madereva wote wanaovunja sheria za
barabarani na kuwachukulia hatua kali.







0 Comments