Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
mamia ya wananchi kabla ya kuzindua Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup
katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano
hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo
yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Chama cha Kuweka na Kukopa (Vicoba-Together) katika sherehe
iliyofanyika Skuli ya Chekechea, Miembeni, Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Mjini, Unguja. Masauni alikichangia chama hicho shilingi milioni tatu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimkabidhi
Mkurugenzi wa Redio ya Coconut mjini Unguja, Zanzibar, Ally Dai, jezi kwa ajili
ya Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup ambayo yamezinduliwa na kiongozi
huyo katika Viwanja vya Matumbaku mjini humo. Mashindano hayo yanawahusisha
wasichana yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya
Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa
kofia) akiyapokea Maandamano ya timu 38 za Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup
katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano
hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo
yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
wanachama wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Vicoba-Together (hawapo pichani)
kabla ya kuzindua kikundi hicho katika sherehe iliyofanyika Skuli ya Chekechea,
Miembeni, Zanzibar. Kushoto ni Katibu wa Vicoba Together, Mwashum Mohammed
Mustafa. Kulia ni Katibu wa Jimbo la Kikwajuni, Kassim Ally Juma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizikagua timu ya
Kikwajuni na Baa kutoka Jimbo la Mtoni kabla ya kuanza Mashindano ya Nage
Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar.
Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo
yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Mchezaji wa Timu ya Kikwajuni, mjini
Unguja, Zanzibar akijaza chupa mchanga wakati wa Mashindano ya Nage Mapinduzi
Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano
hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo
yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani. Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad
Masauni alizindua Mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa)
akiwa katika picha ya pamoja na wanachama
wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Vicoba Together. Masauni alikichangia
chama hicho shilingi milioni tatu.
Picha zote na Felix Mwagara
0 Comments