MKULIMA
na mkazi wa kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Masanze wilaya ya Kilosa
mkoani Morogoro, Augustino Mtitu,amechomwa mkuki mdomoni na kutokea
shingoni.
.....................................................................
Umemjeruhi
hivyo kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro,
kufanyiwa upasuaji kuondoa mkuki huo na kuokoa maisha yake.
Mtitu
na wengine wanane walijeruhiwa katika vurugu zilizohusisha jamii ya
wafugaji wa Kimasai na wakulima wa kijiji hicho kilichopo wilayani
Kilosa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema mpaka jana watu watatu
walikuwa wanashikiliwa na Polisi, na msako unaendelea kuwasaka wale wote
waliohusika katika kufanya vurugu hizo.
Tukio hilo ni la Desemba
25, mwaka huu, baada ya mtu huyo kujaribu kuzuia vurugu hizo,
zilizokuwa zimetokea baada ya wafugaji hao kulisha mifugo yao katika
shamba la maharage na mahindi katika kijiji hicho.
Mtitu
akijaribu kuzuia vurugu hizo, aliishia kuchomwa mkuki na mmoja wa
wafugaji wa jamii hiyo, ambao baada ya tukio hilo walikimbia kutoka eneo
hilo.
Kutokana na tukio hilo, wananchi wenzake waliamua kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya matibabu.
Lakini,
alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya
kufanyiwa upasuaji na matibabu zaidi ya kuokoa maisha yake.
Baada
ya kutokea kwa tukio hilo, muda mfupi baadaye wafugaji hao walirudi
tena kijijini hapo, kwa lengo la kuokoa mifugo yao iliyokuwa imekamatwa,
na ndipo walipoanzisha tena vurugu kwa kuwashambulia watu wengi wanane
akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na wa Kitongoji.
Watu watano,
kati ya waliojeruhiwa, walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Kilosa kupatiwa matibabu. Diwani wa Kata ya Masanze, Bakari Pilo,
akizungumza kwa njia ya simu, alisema hilo ni tukio la tatu kutokea
kwenye kata yake katika kipindi kifupi.
Alisema vitendo hivyo
vinaendelea kuhatarisha usalama wa wananchi, hasa wakulima, kufuatia
mamlaka zinazohusika kushindwa kuwahamishia wafugaji katika eneo
walilokuwa wametengewa, licha ya suala hilo kupitishwa kwenye vikao vya
Baraza la Madiwani.
Stanley Andrea, ambaye ni ndugu wa Mtitu,
yupo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro akimuunguza nduguye,
alisema kuwa tukio hilo ni la Desemba 25, mwaka huu majira ya saa 5
asubuhi kwenye mashamba ya wakulima baada ya wafugaji kuingiza mifugo
kwenye mashamba ya mahindi na maharage ili kulisha mifugo.
Alisema,
wakulima wenye mashamba hayo,waliamua kuifukuza mifugo hiyo, lakini
wafugaji wa jamii ya Kimasai, waliingilia kati na kuanza kuwapiga kwa
fimbo wakulima na kusababisha kutokea kwa vurugu baina ya pande mbili
hizo.
Alisema, mfugaji mmoja wa Kimasai alichukua mkuki na
kumchoma Mtitu sehemu ya mdomoni na kutokezea shingoni na kuwajeruhi
wengine wanane, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji na wa Kitongoji, ambao
baadhi wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.
Alisema kuwa
vurugu ziliongezeka, pale wafugaji hao waliporudi kijijini hapo kwa
ajili ya kuikomboa mifugo yao iliyokuwa inashikiliwa, kabla ya kufika
kwa askari polisi kutoka mjini Kilosa.
Muuguzi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Sanifa Mdee, alisema walimpokea mgonjwa huyo
akiwa na mkuki mdomoni, ulitokea upande wa shingoni na kuanza kumpatia
matibabu na kumtoa mkuki huo, ambapo amelazwa wodi namba moja
hospitalini hapo.
Hata hivyo, alisema kutokana na mkuki huo
kuchomwa kwa nguvu, ulijeruhi baadhi ya meno yake na kuharibu fizi, hali
iliyosababisha jana madaktari kumfanyia upasuaji wa kurekebisha fizi
zake, ambapo baada ya kutolewa mkuki huo, hali yake ilikuwa inaendelea
vizuri.
No comments:
Post a Comment