Mzee
wa Kijiji cha Murangi- Musoma Vijijini, Clifford Biseko (kulia) akifungua rasmi
mkutano wa kujadili uchumi na maendeleo ya Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza
kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo.
Baadhi
ya wananchi wa Musoma Vijijini waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza Mbunge
wao, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo akitambulisha watendaji mbalimbali
kutoka kwenye halmashauri hiyo.
Madiwani
wa Musoma Vijijini wakijitambulisha wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo
na Uchumi ya Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo
hilo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Wadau
wa maendeleo ambao pia ni wazaliwa wa Musoma Vijijini lakini wanaishi nje ya
hapo wakijitambulisha.
.........................................................................................
Wananchi wa Jimbo la
Musoma Vijijini wamempongeza Mbunge wao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo kwa kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ndani ya mwaka mmoja.
Pongezi hizo
zimetolewa na wananchi wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo
na Uchumi ya jimbo uliofanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Murangi, Musoma
Vijijini na kushirikisha wananchi wa jimboni humo, madiwani, wadau wa maendeleo
na watendaji wa Halmashauri husika.
Awali akifungua
mkutano huo mzee wa Kijiji cha Murangi, Musoma Vijijini, Clifford Biseko
alisema wanamusoma vijini wanajivunia maendeleo yanayodhihirika kila kukicha
kutokana na mchango wa mbunge huyo.
Aliongeza kwamba
Profesa Muhongo ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo na kuwa hawajuti kumchagua na
wanamwombea afya njema ili azidi kushirikiana nao katika kusukuma gurudumu la
maendeleo jimboni humo.
Alisema katika
kipindi kifupi cha uongozi wake, wameshuhudia masuala makubwa ya maendeleo kwenye
sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, kilimo, sanaa na michezo.
Akizungumzia suala la
afya, Biseko alisema, Musoma Vijijini haikuwahi kuwa na gari hata moja la
wagonjwa lakini tangu Profesa Muhongo awe Mbunge tayari jimbo hilo linayo magari
manne.
Aliongeza kuwa Musoma
vijijini haikuwahi kupata ugeni wa madaktari bingwa kwa ajili ya vipimo,
ushauri na matibabu lakini kwa Profesa Muhongo hilo liliwezekana kwani
alikaribisha madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi ambao walitoa huduma
bila malipo.
Kuhusu suala la
kilimo, Biseko alisema, tangu Profesa Muhongo achaguliwe, alisambaza tani
kadhaa za mbegu za zao la mihogo na alizeti ili wananchi wajikwamue kwenye
umasikini.
Aliongeza kuwa,
Profesa Muhongo alipeleka wataalamu mahiri wa kilimo kutoka ndani na nje ya
nchi ili kufanya tathmnini ya kilimo bora ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa
kilimo bora.
Aidha, suala la
elimu, Biseko alisema kuwa kulikuwa na uhaba wa madawati 8,000 kwa shule zote
zilizomo jimboni humo na hilo lilitatuliwa bila wao kuchangishwa pia
kusambaziwa shehena ya vitabu vya sayansi kwa shule zote.
Biseko alimalizia kwa
kuzungumzia sekta ya michezo na sanaa alisema kuwa Mbunge ameandaa mashindano mbalimbali
na vilevile kugawa vifaa vya michezo kwenye vijiji mbalimbali jimboni humo jambo
ambalo alisema limehamasisha sekta husika.
No comments:
Post a Comment