Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro wakiendesha Pikipiki kabla ya kuwakabidhi pikipiki hizo vijana 200 wa Jiji la Arusha.
Dereva
wa Bodaboda Dickson Wilbard
akijaribu kuendesha Pikipiki aliyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.
Vijana wa Jiji la Arusha wakiwa na Pikipiki zao walizokabidhiwa na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo (kushoto) pamoja Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Daqarro (kulia) wakimkabidhi Mlemavu Mohamed Issa
(katikati) pikipiki yake aliyopewa kama msaada.
Hizi ndizo Pikipiki aina ya Toyo walizopatiwa vijana 200 wa Jiji
la Arusha.
........................................................................................................................
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo
amekabidhi pikipiki 200 kwa vijana wa umoja wa wandesha Boda boda Jiji la
Arusha (UBOJA) ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu na usiokuwa na riba utakaowawezesha vijana wa kudni hili kujiajiri na kuondokana
na tatizo la ukosefu wa ajira pamoja na umasikini.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Mhe
Gambo amesema kuwa vijana wengi wamekua wakikabiliwa na tatizo la
mtaji hivyo pikipiki hizo zitawasaidia kukuza mitaji yao na kuongeza kipato
chao cha kila siku hivyo kujikwamua katika lindi la umasikini.
Aliongeza kuwa Vijana hao wamekuwa wakipata
Pikipikizi hizi kwa gharama kubwa zaidi kutoka kwa wamiliki binafsi ambapo
inapaswa kulipa mara mbili ya bei ya Pikipiki ndipo unaweza kumiliki au
aendelee kurejesha Fedha siku zote mpaka Pikipiki itakapokufa hivyo kunufaisha
watu wachache ilihali wao wakiendelea kuwa na hali duni kimasiha.
“Nimetambua
jitihada zenu katika kujitafutia kipato na nimesikia mahitaji yenu kupitia
vikoa vyetu tulivyokutana siku za nyuma na nimeona niaze kutatua Changamoto hii
ambayo ndio ilikua kubwa na mengine tunaendelea kuyatafutia ufumbuzi kama Bima
kubwa kwa wote na Bima ya Afya kwa wale ambao hawapo kwenye pango huu” alisema
Gambo.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Boda boda jiji la Arusha (UBOJA)
ameshukuru Uongozi wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Wadhili waliojitolea
kuhakikisha kuwa wanatengeneza fursa za ajira kwa vijana 200 katika jiji la
Arusha jambo ambalo litainua masiha ya vijana walio wengi.
Dereva
wa Bodaboda Dickson Wilbard amesema kuwa mchango huo wa Mkuu wa Mkoa na wa
thamani sana kwa vijana wa Arusha na utawasaidia vijana wengi kuacha kukaa
vijiweni na kujihusisha na vitendo vya uhalifu na badala yake watakua wachapa
kazi.
Pikipikzi
200 zimegharimu Tsh Mil 400 sambamba
na bima kubwa (Comprehensive Insurance)
kwa Pikipiki 200 sawa na Tsh Mil 27 na vijana watapaswa kurejesha Tsh 7000 kwa
siku 305 sawa na Tsh 2,135,000 na watamilikishwa Pikipiki hizo.





0 Comments