Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na mtangazaji wa EATV mara baada ya kuwasili
katika viwanja vya Mlimani City kuhudhulia hafla ya tuzo za Filamu na Muziki za
EATV zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akifuatilia burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa ndani na nje ya nchi wakati wa
hafla ya tuzo za Filamu na Muziki za EATV zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wa muziki wakitoa burudani
katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016)
zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki
na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la
Taifa(BASATA) Bw. Godfrey Muingereza akitoa wito kwawadau kuendelea
kushirikiana na BASATA kufanikisha Tuzo mbalimbali nchini katika hafla ya
utoaji tuzo kwa wanamuziki na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika
Desemba 10, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Romanus
Tairo akitoa rai kwa wasanii wa Filamu nchini kufata sheria na taratibu za uandaaji
na usambazaji wa filamu zao nchini katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki na
wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa tuzo ya heshima kwa Bw. Bonny Kilosa(Dj Bonny
Love) kwa machango wake katika tasnia ya muziki nchini katika hafla ya utoaji tuzo
kwa wanamuziki na wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10,
2016 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la
Taifa(BASATA) Bw. Godfrey Muingereza akitoa tuzo kwa Msanii Ali Kiba ambaye
alichukua Tuzo tatu ikiwemo Wimbo Bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Kiume na Video
Bora ya Mwaka.
Mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Romanus
Tairo akitoa tuzo kwa mshindi wa Filamu Bora ya Mwaka ya Safari ya Gwalu Bw. Gabo
Zigamba.
Baadhi ya mashabiki wa Muziki na filamu
wakifuatilia burudani mbalimbali katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki na
wasanii wa Filamu(EATV Awards 2016) zilizofanyika Desemba 10, 2016 Jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za
Muziki na Filamu EATV 2016.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
.................................................................................
Na
Raymond Mushumbusi WHUSM.
Wadau
wa Sanaa nchini wameshauriwa kujitokeza kudhamini tuzo kwa ajili ya wasanii wa
muziki na filamu nchini ili kuendelea kuzipa nguvu tasnia hizo kwa maendeleo
yake.
Ushauri
huo umetolea jana na wazori wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wasanii wa
muziki na Filamu nchini zilizoandaliwa na kituo cha Televisheni cha East Africa
(Channel 5).
Ameongeza
kuwa wadhamini wengi wajitokeze kwa ili
kuongeza idadi ya tuzo zenye kiwango kinachostahili zenye kuzingatia weledi na
usawa katika utoaji wake.
“Niwaombe
wadau wa sanaa nchini jitokezeeni kudhamini tuzo hizi za filamu na Muziki ili
tuwe na tuzo nyingi zaidi na zenye viwango vya kimataifa”Alisistiza Mhe.
Nnauye.
Kwa
upande wake katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey
Muingereza amesema kuwa BASATA itaendelea kushirikiana na wasanii na wadau wa Sanaa
katika kuandaa na kusimamia tuzo mbalimbali ikiwa ni nia ya Serikali kuikuza
tasnia ya muziki na filamu ambayo ni moja ya tasnia inayoajiri vijana wengi kwa
sasa.
“Nawaalika
wadau wa Sanaa na wasanii wote sisi tuko tayari kushirikiana nao katika
kulisukuma hili guruduma la maendeleo ya Sanaa nchini na nawasahuri tufate tu
utaratibu katiaka kuandaa kazi zenu za sanaa” alisema Bw. Muingereza.
Aidha
mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw.Romanus Tairo amesisitiza wasanii wa
filamu nchini kufata sheria na gtaratibu zote kabla ya kuandaa na kusambaza
filamu zao.
“Nawaomba
wasanii wote wa filamu nchini kufuata Sheria na taratibu zilizopo za kusajili
filamu zote zikakaguliwa na kuoewa kibali cha kuoneshwa sehemu mbalimbali”Alisema
Bw.Tairo.
Tuzo
za Muziki na Filamu za EATV zimeanzishwa kwa dhumuni la kuongeza chachu ya
maendeleo ya tasnia ya muziki na filamu nchini na jumla ya tuzo nane zilitolewa
kwa wasanii wa muziki na filamu na tuzo moja ya heshima ilitolewa kwa msanii
aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia ya muziki nchini Bw. Bonny Kilosa (Dj
Bonny Love).






















0 Comments