Desemba 22,
2016.
Multichoice Tanzania imefanya ziara yake kwenye kituo cha kulelea watoto
yatima cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo mnamo tarehe 22 Desemba.
Kusudi la ziara hiyo, ilikuwa kutoa msaada msimu huu wa krismasi kwa watoto
hao. Baadhi ya viongozi, wafanyakazi wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji wa
Multichoice Tanzania Ndugu Maharage Chande, waliwasilisha zawadi hizo kwa mlezi wa kituo
hicho, aitwaye Mama Kuruthum Yussuph.
Multichoice Tanzania ilimkabidhi mlezi wa kituo cha Al-Madina (Bi Kuruthum)
vifaa mbalimbali vya kuwasaidia watoto hao katika mahitaji yao ya kila siku . Miongoni
mwa zawadi zilizotolewa ni vyombo vipya vya kulia chakula, nguo, vyakula, sare
za wanafunzi wa shule za msingi, vifaa mbalimbali kwa ajili ya mahitaji ya kila siku, pamoja na
kodi ya pango, Jumla ya mahitaji yote yaliyokiabidhiwa leo ikiwa ni ya sh.
Milioni tano (5).
Mnamo mwezi wa sita (6) mwaka huu, Msimu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,
Multichoice Tanzania ilitembelea tena kituo hiki na mojawapo ya mahitaji yaliyopelekwa
ilikuwa ni Vyerehani vinne (4). Siku ya leo mlezi wa kituo Bi Kuruthum Yusufu
ameonyesha eneo la biashara la ushonaji liloanzishwa baada ya kukabidhiwa
vyerehani vile (Pichani). Biashara hii inawasaidia kuwapatia kipato cha kila
siku ambacho husaidia kutimiza baadhi ya mahitaji muhimu ya watoto hawa.
Bi Kuruthum na watoto wa kituo cha
Al-Madina walitoa shukurani zao za dhati kwa msaada uliyotolewa na Multichoice
Tanzania katika kuwasaidia kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Multichoice
Tanzania imekuwa ikisaidia kituo hicho tangia mwaka 2009, mpaka sasa.
Akiwa anakabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Mheshimiwa Maharage
Chande alisisitiza juu ya umuhimu wa kushirikiana na kituo hicho katika
kuwawezesha watoto kusonga mbele kwani ndiyo taifa la kesho, na kila mmoja wetu
ana wajibu wa kujitolea kwa namna moja au nyingine.
...........................................................................
Kwa mawasiliano zaidi:
Instagram (@dstvtanzania), Twitter (@dstvtz), Facebook (https://www.facebook.com/DStvTanzania/), na https://www.dstv.com
Duphney
Mlimuka Karaze
Afisa
Mahusiano
Tel: +255 22 219
9600



0 Comments