Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu na Wananchi pamoja na Watumishi wa Kituo cha Huduma za Sheria, mjini Unguja, Zanzibar (hawapo pichani). Masauni katika hotuba yake, alisema matukio ya unyanyasi yanaongezeka kwa wingi nchini, hivyo amewataka wananchi kujitokeza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji katika vyombo husika kwa wakati. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Prof. Chris Maina Peter na kulia ni Mkurugenzi wa Kituo wa Kituo hicho, Harusi Miraji Mpatani.
Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa anatoa hotuba yake katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu katika Kituo cha Huduma za Sheria, mjini Unguja, Zanzibar. katika hotuba yake, Masauni aliwataka wananchi nchini, kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji katika vyombo husika kwa wakati.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar, Khamis Rashid Kheri baada ya kupokea Matembezi ya kupinga Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto yalioandaliwa na Baraza hilo, Mnarani Mwembe Kisonge, mjini Unguja, Zanzibar. Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas.
Sehemu ya vijana ambao walishiriki Matembezi ya Kupinga Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto wakiwa wameshika bango ambalo lina ujumbe unaowataka askari kuwasaidia wananchi zaidi katika mapambano ya kudhibiti matukio ya unyanyasaji nchini. Vijana hao walipokelewa na mgeni rasmi katika tukio hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa), Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Prof. Chris Maina Peter (wapili kushoto waliokaa), Mkurugenzi wa Kituo wa Kituo hicho, Harusi Miraji Mpatani (wa pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani. Masauni alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ZLSC, mjini Unguja, Zanzibar.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 Comments