Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi
kipya nchini, Ben Poul, amefurahishwa na mafanikio aliyoyapata katika
onesho lake alilolifanya katika mji wa nchini Offenbach Ujerumani,
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kuwasili akitokea nchini Ujerumani,
Poul alisema amepata mafanikio makubwa sana katika onesho lake la nchini
humo, kwa kupata mashabiki wengi ambao hakuwatarajia.
Poul
alisema mafanikio hayo anaweza kusema ni makubwa hasa kwa kufanya
onesho la moja kwa moja katika nchini iliyopo nje ya bara la Afrika na
kupata mafanikio ya aina hiyo.
"Katika maisha
yangu ya muziki ni kitu kikubwa ambacho nimeona hata wadau wangu wa
muziki niwapte ujumbe kuwa nimefanikiwa na onesho langu hilo na
Ujerumani na limenifanya nione kuna mwanga mkubwa kimuziki" alisema
Poul.
Aidha Poul alisema hiyo inatokana na
kufanya onesho akiwa msanii pekee yake kwa kutumia vyombo (live band)
na haikuwa na waafrika ilikuwa na wajerumani na walionesha kukubali
zaidi hit single yake ya ‘Moyo Mashine’.
Alisema
kuwa katika onesho hilo ilihudhuriwa na watu wanaofikia 10,000 na
imeacha historia katika maisha, huku kukiwa na watanzania watatu pekee,
yeye mwenyewe, Emmanuel Austin na mjomba wa Emanuel Austin.
Msanii
huyo alisema katika maisha yake ya muziki onesho hilo ni la tatu kupata
sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki, ikiwa ni pamoja na onesho la Fiesta
lililofanyika Dodoma kwa Wabunge wengi kupata jukwanii na onesho lingine
lilikuwa usiku wa Mwafrika ambalo nalo lilikuwa na watu wengi.
"Narufahia
maisha yangu ya muziki kila siku mashabiki wanakubai nanichofanya na
nyimbo zangu zinapendwa kuchezwa kila kona, lakini kubwa kwangu kwenu
kila mwanamuziki afurahie kazi yake haswa anapoenda sehemu kukubalika na
wenyeji na sio waafrika wenzake ambao uwa wachache ni changamoto ambayo
kila mmoja anatakiwa apambane nayo"alisema Poul.
Msanii
huyoa anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo, Sofia, Moyo Mashine,
Nakuchana, Unanichora’ na hivi karibuni ameshirikishwa kwenye wimbo wa
msanii Darasa ambao umeshika nafasi kubwa ya kupigwa katika vitu
mbalimbali vya radio na televisheni unaitwa Muziki.

0 Comments