Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wakazi wa kijiji
cha Kisorya Wilayani Bunda, mkoani Mara wakati alipotembelea na kukagua kivuko
cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani
hapo.
Mbunge wa Mwibara Mhe.
Kange Rugora (wa pili kushoto), akiongea na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), katika ziara yake mkoani
Mara wakati alipotembelea na kukagua kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma
kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya kilichopo Wilaya ya Bunda.
Meneja wa Wakala wa
Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Eng. Fredinand Mishamo akitoa maelezo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati
alipotembelea na kukagua kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi
Ukerewe na Kisorya wilayani hapo.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akishuka kutoka katika kivuko
cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani
Bunda, wakati alipotembelea na kukagua kivuko hicho.
Muonekano wa kivuko
cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Rugenzi Ukerewe na Kisorya
wilayani Bunda.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua kivuko cha MV Mara
kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Mugara na Kuruge wilayani Bunda, wakati
alipotembelea na kukagua kivuko hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mwl.
Lydia Bupilipili.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akicheza nyimbo za asili za
kabila la wakerewe, wilaya ya Bunda kabla ya kuongea na wakazi wa kijiji cha Iramba,
mkoani Mara.
Muonekano wa kivuko
cha MV Mara kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Mugara na Kuruge, Wilaya ya
Bunda.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akisikiliza kero kutoka kwa mmoja
wa wananchi wa Kijiji cha Iramba, Wilaya ya Bunda, mara baada ya kukagua kivuko
cha MV Mara na kuongea na wananchi hao.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiangalia athari za
miundombinu ya barabara kwenye Daraja la Burendabufwe lilibomoka kutokana na
mvua zilizonyesha hivi karibuni katika barabara ya Kibara-Iramba wilayani Bunda.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewaagiza Wakuu wa
Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini
kuhakikisha wanafuatilia na kusimamia kwa ukaribu utekelezaji
wa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa
kutumia Mfuko wa Barabara katika maeneo yao.
Akizungumza
Wilayani Bunda, mkoani Mara baada ya kupokea taarifa ya hali ya miundombinu Wilayani
hapo, Waziri Prof. Mbarawa amesema kuwa hatua hiyo pia itasaidia kudhibiti upotevu
wa fedha za wananchi pamoja na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
“Nawaagiza
Wakuu wa Wilaya wote na Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia
ipasavyo miradi inayotekelezwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara ambazo ni
fedha za wananchi”, ameagiza Prof. Mbarawa.
Aidha,
amemhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Bunda kuwa Serikali itaendea kufanya kila linalowezekana
kuimarisha miundombinu kwa maendeleo ya watanzania.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mwl.Lydia Bupilipili, amesema kuwa wilaya hiyo
imejiwekea utaratibu wa kufuatilia miradi hiyo lakini pia inawaelimisha
watendaji kata na vijiji kuhusiana na sheria ya barabara.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mbarawa ametembelea Kivuko cha Mv Mara na Mv Ujenzi na
kuahidi kuboresha utoaji wa huduma katika vivuko hivyo ikiwemo ujenzi wa jengo
la abiria katika kijiji cha Iramba na Kisorya.
Amewasisitiza
kudhibiti mapato yatokanayo na vivuko hivyo ili kuweza kuongeza ufanisi na
utendaji wa vivuko hivyo.
Naye,
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mkoani Mara amemhakikishia Waziri
huyo kufunga mifumo ya kielektroniki ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
Aidha,
Waziri Prof. Mbarawa ametembelea barabara ya Busambala - Kisorya (KM 120), na
kutoridhishwa na hatua ya ujenzi wake, hivyo kutoa miezi sita kwa Mkandarasi wa
Kampuni ya ujenzi ya Nyanza Roads Works anayejenga barabara hiyo kukamilisha
ujenzi wake.
Prof.
Mbarawa ameanza ziara yake ya siku mbili mkoani Mara ambapo anatarajia kukagua
miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.
Imetolewa
na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kitengo cha Mawasiliano
Serikalini








0 Comments