Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa
Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili
nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
PICHA
NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi.
Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama
mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee
Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu
Chato mkoani Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi.
Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya
kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la
maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe
Manyama (82) Chato mkoani Geita
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara
baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita
Mdogo wa Marehemu Deodatus Manyama kimshukuru
Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapa pole na kuwafariji kufuatia msiba wa Mpendwa wao
Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika
msiba huo Chato mkoani Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka msibani
mara baada ya kutoa pole.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29
Desemba, 2016 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita kutoa pole
kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni mzee maarufu
wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni jirani yake.
Rais
Magufuli pamoja na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa kuondokewa na
mpendwa wao pia amitaka familia ya mzee Manyama kuendelea kuishi kwa kushikamana
na kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa marehemu na kuwataka kuepukana na
mifarakano.
''Unapotokea
msiba kama huu katika familia nyingi huzuka mifarakano, ombi langu kwenu wewe
Mama mkubwa na Mama mdogo kamwe msikubali kufarakanishwa kutokana na kifo cha
mume wenu,muwaongoze watoto wenu ili muendelee kuishi kwa kupendana kama enzi
za uhai wa mzee''
Aidha
Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Mzee Manyama kuwa alikuwa mzee maarufu kijijini
hapa na miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo ambaye pia alimshonea sare
zake za shule wakati akisoma.
Kwa
upande wake Mdogo wa marehemu ambaye ni msemaji wa familia Bwana Deodatus
Manyama ambaye ni msemaji wa familia amemshukuru Rais Magufuli pamoja na ujumbe
wake alioambatana nao kuwapa pole katika msiba huo, na kwamba kitendo hicho
kinaonyesha kuwa Rais magufuli si mtu asiejikweza wala asiye na majivuno.
Marehemu
Mzee Admirabilis Mbabe Manyama amefariki akiwa na umri wa miaka 80,ameacha
wajane wawili,watoto 15 na wajukuuu kadhaa.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita.
29 Desemba, 2016









0 Comments