Kaimu
Mnikulu Ngusa Samike akimkabidhi Bi Sauda Kasimu fedha tasilumu kiasi cha
shilingi milioni tano kama mchango wa Mh
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli toka kwenye mshahara wake,kwa ajili ya
mahitaji ya mototo wake Haidari Bonge anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama
mwili. Kulia kwa Bi. Sauda Kassim ni Dr Andrew
Foyi Daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi
toka Hosipitali ya Taifa Muhimbili.
Bi
Sauda Kasimu akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea fedha
tasilumu kiasi cha shilingi milioni tano kutoka kwenye mshahara wa Mhe. Rais
Magufuli na kwa ajili ya mahitaji ya mototo Haidari Bonge anayesumbuliwa na
tatizo la kuota nyama mwilini. Bi. Sauda Kassim amemshukuru Mhe Rais kwa msaada
huo na kuomba Watanzania wengine kuendelea kumsaidia kijana wake.
Afisa
mawasilioano na Huduma kwa wateja toka benki ya CRDB Bw Godwin Semunyu
akimkabidhi kiasi cha Shilingi laki tano Bi Sauda Kasimu ili kuunga mkono hatua ya Mh Rais Magufuli
ya kutoa sehemu ya mshahara wake kiasi cha shilingi milioni tano za kuweza
kumsaidia mtoto Haidari Bonge anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama mwilini.
Bi
Sauda Kassim akiweka saini kwenye kadi ya mashine za kutolea fedha (ATM) mara baada ya kukamilisha zoezi la kufungua
akaunti ya benki katika tawi la CRDB Azikiwe jijini Dar es salaam itakayokuwa
ikitumiwa na wasamaria wema kuweza kupokelea michango mbalimbali kwa ajili ya
kumhudumia mtoto wake Haidari Bonge anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama
mwilini. Akaunti hiyo ni namba 01522336450100 SAUDA KASSIMU tawi la Azikiwe
(Picha zote na IKULU)
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli leo
tarehe 5 Desemba, 2016 wamekabidhi msaada wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya
kusaidia matibabu ya mtoto Haidari Bonge mwenye umri wa miaka 9 anayesumbuliwa
na tatizo la kuota nyama kichwani, kinywani na machoni.
Fedha hizo
zimekabidhiwa kwa Mama wa mtoto huyo Sauda Kassim na Kaimu Mnikulu Ndugu Ngusa Samike kwa niaba ya Rais Dokta Magufuli katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili ambapo mtoto huyo anapatiwa matibabu.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhi fedha hizo, Kaimu Mnikulu Ndugu Ngusa Samike amesema Rais Dkt. Magufuli ameguswa baada
ya kutazama kipengele cha Hadubini “Habari
kwa Kina” kilichorushwa hewani katika taarifa ya habari saa 2 usiku na
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) tarehe 03 Desemba, 2016.
Kwa upande wake
Daktari Bingwa wa magonjwa ya ngozi Dkt. Andrew Foi amesema mtoto Haidari anayeishi
Mbagala Kuu Jijini Dar es Salaam alianza kuota nyama miezi mitatu baada ya
kuzaliwa na amekuwa akifanyiwa upasuaji wa kuondoa nyama hizo mara kwa mara.
Dkt. Foi amesema
Hospitali ya Taifa Muhimbili inatoa matibabu ya mtoto huyo bure tangu awasili
hospitalini hapo isipokuwa kwa matibabu ambayo hayapatikani hospitalini hapo
ndio analazimika kuyalipia katika sehemu husika.
Amesema mtoto
Haidari anahitaji eneo maalum la kuishi muda wote ambalo lina giza na kuvaa
nguo nyeusi zinazomfunika mwili wote ili kujikinga na miale ya jua ambayo
imekuwa ikimuathiri kwa kiasi kikubwa.
Mama wa mtoto
Haidari, Ndugu Sauda Kassim amemshukuru
Rais Dkt. Magufuli na mke wake Mama Janeth Magufuli kwa moyo wa upendo waliouonesha
baada ya kuguswa na shida zinazomkabili mtoto wake na kutoa msaada huo na hivyo
kuomba wananchi wengine waige mfano wa Rais na Mkewe katika kumsaidia mwanawe.
Tayari mtoto
Haidari Bonge, ameshafunguliwa akaunti
katika Benki ya CRDB tawi la Azikiwe yenye namba 0152236450100, ambapo benki hiyo kupitia kwa meneja Uhusiano wake
Godwin Semunyu amekabidhi shilingi laki Tano ikiwa ni msaada kutoka Benki hiyo.
Jaffar
Haniu
Naibu Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
05
Desemba, 2016
0 Comments