Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
habari kuhusu mwandishi wa kituo cha ITV Halfani Liundi aliyekamatwa
hivi karibuni na jeshi la polisi, ambapo pamoja na mambo mengine
alisema kuwa anatambua umuhimu wa vyombo vya habari na hivyo mwandishi
anauhuru wa kwenda popote kupata taarifa yeyote kwa kuzingatia misingi
ya uandishi wa habari.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari
wa Mkoa wa Arushaa ofisini kwake juzi kutoka vyombo mbalimba vya habari
kuhusu sakata la kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa kituo cha
televisheni cha ITV Halfani Liundi ambapo amehaidi kulishughulikia huku
akiwataka waandishi kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya uandishi
wa habari.
Mwandishi wa habari wa kituo cha channel Ten Aristrides Dotto akichangia
katika mkutano huo wa waandishi wa habari na mkuu wa Mkoa juzi ofisinii
kwake jijini Arusha.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Mosses Mashalla akichangia katika
mkutano huo wa mkuu wa Mkoa na waandishi wa habari mkoa wa Arusha.
(Picha
na Pamela Mollel)
No comments:
Post a Comment