TAASISI YA BO's LOVE YA NCHINI CHINA YATOA MIL25.2 NA VYAKULA KUSAIDIA KITUO CHA KULEA WATOTO YATIMA CHA MSIMBAZI CENTRE - MTAZAMO MEDIA

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 26 December 2016

TAASISI YA BO's LOVE YA NCHINI CHINA YATOA MIL25.2 NA VYAKULA KUSAIDIA KITUO CHA KULEA WATOTO YATIMA CHA MSIMBAZI CENTRE

 Mkuu wa kituo cha kulea watoto cha Msimbazi Centre, Anna Francis ,aliyebeba mtoto akiwa na wageni waliotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya vyakula na fedha.
(picha na Mwamvua Mwinyi)
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Bo’s aitwae Bo Sun aliyebeba mtoto wa kituo cha kulea watoto cha Msimbazi akiwa na baadhi ya wageni waliojitolea michango kwa ajili ya kukisaidia kituo hicho wakiwa katika picha ya pamoja.

 Mwenyekiti wa Taasisi ya Bo’s aitwae Bo Sun katikati akimkabidhi Anna Fraancis mkuu wa kituo cha kulea watoto cha Msimbazi sehemu ya fedha zikiwa ndani ya bahasha kulia ni Sara Hong mmoja wa wanachama wa kujitolea wa taasisi hiyo.
 Baadhi ya wageni waliojitokeza kutoa fedha kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto yatima cha Msimbazi Centre wakimkabidhi mkuu wa kituo hicho Anna Francis katikati ni mwenyekiti wa Taasisi ya B’os Bo Sun akishuhudia.
Baadhi ya watoto wakiwa na walezi wao kwenye kituo hicho cha kulea watoto cha Msimbazi Centre.  (picha na Mwamvua Mwinyi) 
.........................................................................................................
Na Mwamvua Mwinyi

TAASISI ya misaada ya Bo’s Love Childrens Home Foundation kutoka nchi ya China imetoa msaada wa kiasi cha sh.mil 25 .2 pamoja na vyakula katika kituo cha kulea watoto cha Msimbazi centre kilichopo Jijini Dar es Salaam .

Msaada huo unalenga kuwaondoa watoto hao kwenye majonzi ya kujiona wapweke katika sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwemo X-mass na mwaka mpya 2017.

Akikabidhi fedha na vyakula hivyo,juzi kwenye kituo hicho ,mwenyekiti wa shirika hilo aitwae ,Bo Sun alisema wakati wakisheherekea uzinduzi wa taasisi hiyo wameamua kutoa msaada kituoni hapo kwa ajili ya watoto.
Sun alieleza kuwa awali walitembelea na kuona namna watoto hao wanavyolelewa hivyo na kubaini kituo hicho kinahitaji misaada ya hali na mali .
“Mbali ya kuzindua taasisi yetu hii lakini tumekuwa tukisaidia vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima na watu wanaotusaidia wamekuwa wakichanga fedha kwa ajili hiyo ili watoto hao wafarijike
,” alisema Sun.

Hata hivyo,Sun alifafanua kwamba fedha zilizotolewa ni michango ya wafanyabiashara mbalimbali wa China ambao wako hapa nchini ambao wameguswa kusaidia kituo hicho.

“Wapo wawakilishi wataendelea kukisaidia kituo hiki na tunaomba na watu wengine wajitokeze kusaidia watoto hawa kwani kutoa ni moyo na sio utajiri,” alisema Sun.

Akishukuru kupatiwa misaada hiyo ya chakula na fedha taslimu sh.mil 25.2,mkuu wa kituo hicho cha kulea watoto ,Anna Francis .aliishukuru taasisi hiyo kwa kuonyesha ujali.
Alieleza changamoto kubwa waliyonayo ni fedha kwa ajaili ya kuwalipa mishahara watumishi 24 ambao wanawahudumia watoto waliopo kwenye kituo chake.

“Tuna watoto 52 na tunawashukuru watu kama hawa wanaokuja kutusaidia kwani fedha hizi hutusaidia hata kuwauguza magonjwa mbalimbali hawa watoto wakati wakiuguara,” alisema Anna.

Anna alibainisha,kituo hicho huwa kikiwatibia watoto hao na kuwahudumia malazi na mahitaji yote muhimu huku watoto hao wakiwa wakishikwa na magonjwa mbalimbali kutokana na kuwa bado ni wadogo .


Aliiomba serikali na wadau mbalimbali wajitokeze ili kuisaidia hasa kwa upande wa matibabu .

 Kituo cha kulele watoto yatima cha Msimbazi Centre,kilianza kutoa huduma hizo mwaka 1968 na kina hudumia watoto wenye umri kuanzia siku mmoja hadi miaka mitatu ambao wanatupwa na wazazi wao.   

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages