Idadi
ya Watu wazima wanaotumia huduma za kifedha kupitia simu za mkononi imeongezeka
kutoka asilimia 61 ya mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 80 ya mwaka 2016.
Akiongea
wakati akiwasilisha matokeo ya tafiti ya matumizi ya huduma rasmi za kifedha nchini Meneja Mradi wa Sauti za Wananchi kutoka
asasi ya TWAWEZA Nellie Njovu alisema kuwa ongezeko hilo limevuka lengo la
serikali waliojiwekea kufikisha huduma za kifedha kwa asilimia 50 ya watanzania
ifikapo 2016.
Aidha
Bi. Nellie alisema kuwa asilimia 80 ya watumiaji wa huduma za kifedha kupitia
mitandao ya simu wamesema wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na ni mtumiaji
mmoja kati ya kumi anayesema haridhishwi na huduma hizo.
Matokeo
haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutpka kwa wahojiwa 1800 kutoka
maeneo mbalimbali Nchini kati ya terehe 14 hadi 26 septemba 2016.
0 Comments