Msimamizi
wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi II, Mhandisi
Bernd Siegemund akitoa maelezo ya historia ya mradi huo kwa maofisa wa ukaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakati wataalam hao walipofanya
ziara kukagua maendeleo ya ujezi wa kituo hicho.
Msimamizi
wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi II, Mhandisi
Bernd Siegemund akiweka bayana mipango na mikakati ya kumalizika kwa ujenzi wa kituo cha kuzalisha
umeme cha Kinyerezi II katika muda uliopangwa. Wengine ni wataalam kutoka Tume
ya Mipango, wataalam kutoka TANESCO pamoja na wahandisi wanaotekeleza mradi
huo.
Mhandisi
Omari Athuman (aliyeshika notebook) kutoka Tume ya Mipango akitoa ushauri kwa
mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha kinyerezi II.
Picha
ya pamoja kati ya wataalamu kutoka Tume ya Mipango, wataalam kutoka TANESCO
pamoja na wahandisi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme
cha kinyerezi II.
Shughuli za ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha kinyerezi II
zikiendelea.
Moja
ya sehemu ziliyojengwa kwa ajili ya kusimika mitambo ya kuzalisha umeme.
...............................................................................
Na
Adili Mhina, Dar
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Tume ya Mipango imetembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha
kuzalisha umeme cha Kinyerezi II kwa lengo la kuangalia maendeleo ya kituo
hicho ambacho kinatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati 240 pale
kitakapokamilika.
Akizungumzia juu ya
maendeleo ya mradi huo, msimamizi wa shughuli za ujenzi katika kituo hicho,
Mhandisi Bernd Siegemund kutoka Ujermani alieleza kuwa ujenzi wa kinyerezi II unaendelea
vizuri na unatarajia kukamilika kwa muda uliopangwa.
Ujenzi huo ulianza tarehe 13
Machi, 2015 na kutokana na kasi yake, Mhandisi Siegemund alieleza kuwa
matarajio ni kwamba hadi kufikia mwezi Novemba mwaka 2017 mtambo wa kwanza utaanza
kuzalisha umeme huku mitambo mingine ikiendelea kuwashwa kadiri itakavyokuwa
inakamilika.
Kuhusu vifaa vya ujenzi vinavyohitajika,
Mhandisi Siegemund alisema kuwa wanajitahidi kununulia ndani ya nchi vifaa
vyote vinavyopatikana na vinavyokidhi mahitaji katika mradi huo na pale
inapobidi hulazimika kuagiza kutoka nje.
Aliongeza kuwa pamoja na
nondo kuzalishwa ndani ya nchi wamelazimika kuagiza kutoka nje kwa kuwa viwanda
vya ndani bado havijazalisha aina ya nondo wanayohitaji katika ujenzi wa kituo
hicho.
“Vifaa kama saruji na
vingine tunaagiza kutoka kwa wazalishaji wa ndani ili kusaidia kukua kwa uchumi
wa nchi. Tulitaka kuagiza nondo hapa nchini lakini hatukupata kiwango tunachohitaji
kwa kuwa ujenzi huu hautumii nondo tulizozizoea katika ujenzi wa kawaida,”alieleza
Siegemund.
Aliongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utakabidhiwa na
kuendeshwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ambapo wataalam wa shirika hilo
wanaendelea kupata elimu na uzoefu katika kutumia mitambo ya kisasa zaidi na
wanashirikishwa katika kila hatua ya ujenzi wa kituo hicho.
Wataalam kutoka Tume ya
Mipango walipata fursa ya kukagua maeneo mbalimbali ya mradi huo ambao
umesaidia kupatikana kwa ajira takriban 400 katika ngazi mbalimbali na
kumshauri mkandarasi huyo kuendelea na kasi hiyo ili malengo ya Mpango wa Pili
wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) pamoja na Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2025 yafikiwe kwa haraka.







0 Comments