Meya mteule wa manispaa ya
Kigamboni mhe. Maabadi Sulemani Hoja aliye simama akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa Meya.
.........................................................................................
Na John Luhende mwambawahabari
Uchaguzi wa Meta na Naibu Meya wa manispaa ya Kigamboni umefanyika kwa
amani na utulivu ambapo wagombea wa chama cha Mapinduzi CCM wameibuka na
ushindi wa nafasi zote mbili.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mwenyekiti wa uchaguzi
huo ambaye pia ni katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Muhando
amemtangaza Diwani wa kata ya Pembamnazi
Mhe. Maabadi Suleiman Hoja (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha Meya baada ya
kupata kura 9 na kumshinda Mgombea Celestine Maufi wa CHADEMA aliye pata
kura 5 kati ya kura zote 15 ambapo Kura moja iliharibika.
Kwa upande wa nafasi ya Naibu meya Mhe. Amin Mzuri Sambo
Diwani wa kata Kibada ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 10 na kumbwaga
mpinzani wake Mhe. Ernest Mafimbo (CUF) aliyepata kura 5 katiya
kura zote 15 zilizopigwa.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi Meya mteule Maabadi Selemani hoja
amewashukuru wapigakura wote walioshiriki uchaguzi huo na ameahidi kufanya kazi
kwa ushirikiano bila ubaguzi wa vyama ili kuleta Maendeleo kwa wananchi
wa Kigamboni.
Naye aliye kuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Meya kwa upande wa
UKAWA akiwakilisha Chama Cha wananchi CUF, Ernest Ndamo Mafimbo ,
ameuelezea uchaguzi huo kuwa. Ulikuwa huru na haki nakukubali kushindwa
nakuahidi kushirikiana na washindi hao ili kuwa tumikia wananchi.
"Tumekubali wenzetu wameshinda maana hata idadi yetu
sisi ilikuwa ndogo wao wlikuwa 10 na sisi tulikuwa 5 tu kwa hiyo
unaweza kuona jinsi mambo yalivyokuwa "
Mbunge wa Kigamboni Dr Faustine Ndungulile , akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa uchaguzi amesema nimuda Sasa wakufanyakazi kwa kuwa mambo mengi yalisimama
kwa muda mrefu kwa kukosa baraza la madiwani kwa kwaajili kupitisha
mipango na miradi mbalimbali ya Maendeleo.

0 Comments