Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu
Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya
Ustawishaji wa makao makuu(CDA) Dodoma na mkandarasi kwa pamoja wanasimamia
mradi wa ukarabati wa makazi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika eneo
la kikuyu mkoani Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu
Mhe.Jenista Mhagama akiongea jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na
Rasilimali watu kutoka wizara hiyo Issa Nchasi wakati akikagua ujenzi wa makazi
ya waziri mkuu Mkoani Dodoma.Nyuma ni moja ya ofisi ambayo imekamilika.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu
Mhe.Jenista Mhagama akimskiliza Mhandisi Mhandisi Joseph Muhamba kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
juu ya maendeleo ya ujenzi wa Makazi ya Mhe.Waziri Mkuu.Wengine ni Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu kutoka wizara hiyo Issa Nchasi na
Mkurugenzi msaidizi wa Idara hiyo Samwel
Mwashambwa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu
Mhe.Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Joseph Muhamba kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
wakati Waziri uyo alipotembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa makazi
ya Waziri mkuu eneo la Mlimwa,Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu
Mhe.Jenista Mhagama akiangalia maendeleo ya ujenzi wa Barabara na Madaraja katika Ofisi mpya Waziri Mkuu iliyopo eneo
la Mlimwa,Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu
Mhe.Jenista Mhagama akikagua ujenzi wa
tanki la kuhifadhi na kupeleka maji katika makazi ya waziri Mkuu eneo la
Mlimwa,Dodoma.Tenki hilo lina uwezo wa kuhifadhi lita laki mbili kwa siku.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
................................................................................................................
Na Daudi
Manongi-MANONGI
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Mhe.Jenista Mhagama
amemwagiza mkandarasi anayesimamia ukarabati wa nyumba watakazo ishi watumishi
wake kukabidhi nyumba hizo ifikapo tarehe 28 Mwezi huu.
Ameyasema hayo wakati
akikagua ukarabati wa makazi ya watumishi
wake yaliyopo eneo la kikuyu mkoani Dodoma yanayosimamamiwa na Mamlaka ya
Ustawishaji wa makao makuu Dodoma(CDA).
“Kama wote mnakumbuka
agizo la mheshimiwa Waziri mkuu kwamba kufikia mwezi Februari mwakani Mawaziri
wote,Manaibu Waziri,Makatibu wakuu na Manaibu wake pamoja na sehemu ya
watumishi wachache wa kila wizara lazima wawe wameshafika Dodoma na leo tupo
hapa kuhakikisha miundombinu iko sawa tayari kwa kazi ambayo tunataka kuifanya
tukiwa hapa Dodoma,”Alisema Mhe.Mhagama
Aidha amesema kuwa
nyumba hizo zimefikia katika hatua nzuri sana na hivyo ikifika februari wataanza
kuhamia kama ilivyoagizwa.
Pia Waziri Mhagama
amesema kuwa Ujenzi wa makazi ya Waziri Mkuu pia yamefikia hatua nzuri ambapo
kwa sasa wanakamilisha uwekwaji wa tenki la maji ambalo litasaidia kuhifadhi
lita laki mbili kwa siku kwa ajili ya matumizi ya kila siku na pia ujenzi wa barabara mbili
zinazofika Ofisi ya Waziri Mkuu mkandarasi ameshakamilisha ujenzi wa barabara
hizo tayari kwa matumizi.
0 Comments