Na: Frank Shija – MAELEZO
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa
kuwa mgeni katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania
(TAWJA).
Hayo
yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Chama hicho Jaji C. W. Makuru leo jijini Dar es Salaam
ambapo katika taaarifa hiyo imesema kuwa
mkutano huo utafanyika siku ya jumamosi, tarehe 07/01/2017 katika ukumbi wa
PSPF Goldeni Jubilee Tower ghorofa ya nne.
Aidha taarifa hiyo
imeongeza kuwa Mkutano huo utatanguliwa na mafunzo ya uandishi wa hukumu na elimu
kuhusu mifuko ya jamii.
Kwa mujibu wa taarifa
hiyo mkutano huo unatarajiwa kuudhuriwa na wa wanachama ambao ni Mahakimu na
Majaji 200 kutoka pande zote za Tanzania.

0 Comments